Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe amemtaka
Mkuu wa Wilaya ya Singida kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya kuhamishia
makao makuu ya halmashauri ya Singida katika mji mdogo wa Ilongero
ndani ya kipindi cha miezi sita ili kusogeza huduma karibu na wananchi
wa halmashauri hiyo.
Mheshimiwa
Mhandisi Mtigumwe amefikia uamuzi huo kutokana na taarifa za kuwepo
watu wachache wanaotaka kufanya mabadiliko ya makao makuu bila ya
kusikiliza mawazo ya wananchi wengi huku wananchi wakipendelea makao
makuu ya halmashauri hiyo kuwa katika mji mdogo wa Ilongero.
Ameongeza
kuwa baraza la madiwani la halmashauri ya Singida linapaswa kuketi tena
na kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya wananchi wengi huku akiongeza
kuwa endapo wanataka kufanya mabadiliko wayafanye wakiwa tayari
wameshahamia katika halmashauri yao tofauti na sasa ambapo bado ofisi
zipo manispaa ya Singida.
Mheshimiwa
Mhandisi Mtigumwe amesema wananchi wanataka kupatiwa huduma kwa ukaribu
hivyo halmashauri kuhamishiwa Ilongero itasaidia kusogeza Huduma ambapo
zitatolewa kwa ufanisi huku akimshauri Mkurugenzi wa halmashauri hiyo
kujipanga ndani ya kipindi hicho waanze kutumia ofisi chache zilizopo.
Aidha
Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amewataka wananchi wa halmashauri na Mkoa
mzima wa Singida kujituma na kufanya kazi kwa bidii, wakulima wajiandae
FEMA kwa msimu huu wa kilimo na kujitahidi kutunza vyakula ili
kujiepusha na njaa na wafanyabiashara watumie fursa mbalimbali
kujiongezea kipato.
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Martha Mlata
amesema chama hicho mkono mapendekezo ya wananchi yakutaka makao makuu
kuwa katika mji mdogo wa Ilongero na kuahidi kufuatilia na kusimamia
utekelezaji wake.
Katika
kuunga mkono mapendekezo ya wananchi Mbunge wa jumbo la Singida
kaskazini la kaskazini Mhe. Lazaro Nyalandu amesema kufikia mwezi
Januari ataweka ofisi za Mbunge katika mji wa I'll wananchi wapate
Huduma na kumfikishia kero kwa ukaribu zaidi.
0 comments:
Post a Comment