Na Evelyn Mkokoi-Singida
Wamilki wa Leseni za uchimaji mdogo
wa madini wa Joshua Mine na Sekeknke one mine wa Sekenke Mkoani Singida,
wametozwa faini ya shilingi milioni 10 kila moja kwa kosa la uchafuzi wa
mazingira wa kutumia vibaya madini ya zebaki, hivyo kuhatarisha maisha ya
viumbe hai.
Baraza la taifa la Hifadhi na
usimamizi wa Mazingira limeitoza faini hiyo kupitia mratibuwa wa Barazakanda a
Ziwa Bw. Jamali Baruti na kiwataka wamiliki hao kulipa faini hiyo ndani ya siku
14.
Adhabu hiyo inatokana na makelele
katika eneo la uchimbaji, kusambaa kwa vumbi lisilovumilika, kukosekana kwa
vyoo pia na matumizi mabaya ya miti katika uchimbaji wao ambao huenda sambamba
na uharifu wa misitu.
Aidha Baraza limewataka wachimbaji
hao kuwa na vyeti vya tathmini ya athari ya mazingira pamoja na leseni ya
uchimbaji.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wiaya ya
Mkalama Injinia Joakim Masakala
akimuwaklisha mkuu wawiaya ya Iramba, alisema kuwa ni vizuri wakazi wa
maeneo hayo wanavyojibidisha katika kazi lakini ni muhimu sana kuzingatia afya
kwani uchimbaji wa kutumia madini aina ya zebaki bila vifaa salama kazini
unaweza kuleta maradhi hususan ya saratani kwani madini hayo upenya kirahisi
katika mwili wa binadamu.
Awali Katika Kikao na uongozi wa Mkoa
pamoja na wadau wa Mazingira Naibu Waziri Mpina alitolea ufafanuzi masuala
mbalimbali ya Mazingira ikiwemo matumizi ya Mifuko ya plastic na kuwashauri
wakazi wa singida kutunza mazingira akitolea mfano wa ziwa Kitangiri lililoo
Hatarini kutoweka kabisa.
0 comments:
Post a Comment