Na Nathaniel Limu- Singida
Waziri
 wa mambo ya ndani Mhe. Mwigullu Lameck Nchemba (mb), ameliagiza jeshi 
la polisi nchini,kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria  
madereva wanaoacha mawe na matawi ya miti barabarani.
Nchemba
 ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Iramba mkoani Singida, ametoa agizo 
hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha 38 cha bodi ya barabara mkoa 
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini 
hapa.
Amesema
 baadhi ya madereva wa magari na hasa yale makubwa,hutumia mawe kuzuia 
magari yao kutembea wakati wakiyafanyia matengenezo ya dharura.
“Wakiisha
 maliza kuyafanyia matengenezo magari yao, madereva hao huyaacha 
barabarani mawe na matawi ya miti ambayo hutumika kutoa tahadhari kwa 
vyombo vingine vya moto. Kitendo hicho kinahatarisha maisha na mali 
za watumiaji wengine wa barabara kwa vile yanaweza kusababisha ajali”, 
amesema Mwigullu.
Kwa
 hali hiyo amesema jeshi la polisi linapaswa kuimarisha mawasiliano ili 
waweze kuwathibiti na kuwakamata madereva wanaoacha mawe na matawi ya 
miti barabarani.
Katika
 hatua nyingine, waziri huyo amesema upo umuhimu mkubwa wa wananchi na 
hasa wale wanaoishi kando kando ya barabara kuelimishwa juu ya matumizi 
bora ya barabara zinazojengwa kwa fedha nyingi ili waweze kuacha 
kupitisha mifugo yao na mikokoteni barabarani.
Kwa
 upande wake mwenyekiti wa bodi ya barabara na Mkuu wa Mkoa wa Singida 
Mhandisi Mathew John Mtigumwe ameagiza kuwa fedha zinazotolewa na 
serikali na wafadhili mbalimbali wa miradi ya barabara matumizi yake 
yasimamiwe kikamilifu, ili zitumike kwa miradi iliyokusudiwa.
“Ujenzi
 wa miradi hiyo ya barabara ufanane na thamani halisi ya fedha 
zilizotumika. Pia kazi za ujenzi wa barabara za ngazi zote wapewe 
wakandarasi bora na wenye uwezo wa kutekeleza miradi ikakamilika kwa 
wakati. Nasisitiza kuimarishwa kwa usimamizi na ukaguzi wa mara kwa mara
 wa miradi ya barabara ili ziwe za kiwango kinachokusudiwa”,amesema.
Wakati
 huo huo, mhandisi Mtigumwe ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa 
alikuwa meneja TANROADS mkoa, ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa 
TANROADS mkoa wa Singida chini ya meneja wake Mhandisi Leonard Kapongo 
kwa kazi nzuri ya usimamizi na ukaguzi uliopelekea miradi ya barabara 
kujengwa kwa ubora unaofafana na fedha zilizotumika.
0 comments:
Post a Comment