Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Daktari bingwa wa macho Mkoani Singida Ngh'ungu Kuzenza
akimfanyia uchnguzi wa macho mgonjwa wa kisukari katika kuadhimisha siku
ya kisukari duniani.
Na Grace Singida
Wagonjwa
wa kisukari Mkoani Singida leo wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya
macho na daktari bingwa wa macho katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa
kisukari duniani ikiwa na kauli mbiu ya ugonjwa wa kisukari na magonjwa
ya macho.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida Dokta Ramadhani
Kabala amewaambia wagonjwa wa kisukari waliohudhuria kufanyiwa uchunguzi
wa macho kuwa maadhimisho hayo mwaka huu yamelenga kuzuia wagonjwa
wasiathirike zaidi na magonjwa yatokanayo kisukari.
Dokta
Kabala amesema ugonjwa wa kisukari hushambulia zaidi macho, figo na
moyo hivyo serikali imeweka mkazo wa kuwafanyia uchunguzi ili kubaini
tatizo ili wapatiwe matibabu mapema au kuzuia yasitokee kabisa kwa
kufuata kanuni na taratibu za ugonjwa huo.
Ameongeza
kuwa ugonjwa wa kisukari unawakumbusha watu kuishi kwa kufuata kanuni
bora za afya kama kula mlo kamili, kula matunda badala ya juisi
zilizotengenezwa viwandani, kufanya mazoezi na kupunguza vilevi na
sigara hivyo wagonjwa wa kisukari hawana togauti na watu wengine
isipokuwa wao hushauriwa kufuata kanuni hizo kwa umakini mkubwa.
Dokta
Kabala amewakumbusha kutumia dawa kwa kufuata usahuri wa daktari wao
pamoja na kuhudhuria kliniki za kisukari kwakuwa kliniki hizo
zinawasaidia katika kushauriana namna bora ya kuishi kwa kufuata
masharti wananyopewa pamoja kuelimishanzaidi juu ya ugonjwa huo.
Naye
Daktari bongwa wa macho Mkoani Singida Dokta Ngh’ungu Kuzenza amesema
utaratibu huo unasaidia kuzuia au kupunguza madhara ya ugonjwa wa
kisukari kwakuwa wengi watatambuliwa kabla hawajafikia hatua ya
kupofuka.
Dokta
Kuzenza ameongeza kuwa changamoto kubwa ni watu wengi kutopima ugonjwa
wa kisukari mapema mpaka wanapougua na hivyo kujikuta wameshaathirika
macho ndipo hutafuta huduma.
Kwa
upande wake mmoja kati ya wagonjwa wa kisukari 76 waliopata huduma ya
kibingwa ya macho Bi Asha Selemani Waziri Mkazi wa Iguguno ameema
serikali imeweka utaratibu mzuri wa kuwapima macho ili waweze kupata
tiba mapema.
Bi
Waziri ameiomba serikali kuendelea kuweka utaratibu wa kuwapima
wagonjwa wa kisukari magonjwa mbalimbali kama moyo na figo huku
akiwashauri wagonjwa wa kisukari kufuata ushauri wanaopewa na wataalamu wa afya.
0 comments:
Post a Comment