Na Evelyn
Mkokoi – Singida
Katika kutekeleza agizo la Serikali
la usafi wa mazingira kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi, wananchi wa Mkoa wa
Singida wamejitokeza kwa kwingi katika zoezi hilo lililofanyika kitaifa mwezi
huu mkoani humo.
Akishiriki zoezi hilo Mkoani Singida kitaifa, Naibu waziri Ofisi ya
Makamu w Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameupongeza uongozi wa
Mkoa wa Singida na wana singida kwa
ujumla kwa jitihada walizoonyesha kwani kila eneo la Singida Jumamosi ya leo
Limeonekana kuwa nadhifu kabla hata ya muda wa kuanza kufanya usafi tofauti na
mikoa mingine ambayo amewahi kushiriki zoeZi hilo.
Akiongea na Hadhara iliyojitokeza
katika siku ya usafi Mjini Singida Leo, Mpina alisema kuwa usafi wa
mazingira unapunguza magonjwa yatokanayo
na uchafu akitolea mfano ugonjwa wa kipindu pindu na hivyo taifa likiwa safi
litaweza kuokoa ngumukazi yake, na kupunguza gharama ambazo zingetumika kutibu
maradhi hayo.
“Ukiona Msichana mzuri barabarani
ujue kagharamiwa ukiona kijana mtanashati vilevile ujue kagharamiwa Mkiona
taifa zuri na safi ujue limegharamiwa na wananchi wake wamejipanga vizuri,
hivyo wana singida Muendelee kujitahidi katika suala zima la usafiwa
mazingira.” Alisisitiza Mpina.
Zoezi la usafi wa Mazingira Mkoani
Singida lilienda sambamba na zoezi la upandaji miti ambapo, Naibu Waziri Mpina
Pia alishiriki na wananchi katika zoezi
la kupanda miti mkoani Singida ambapo alipanda mti aina ya mpararachichi katika
eneo la stand mpya ya Misuna.
0 comments:
Post a Comment