Na. Lilian Lundo – MAELEZO
Dar es Salaam
28.11.2016
IMEELEZWA
kuwa Uongozi bora na matumizi bora katika usimamizi wa fedha za
Serikali ni miongoni mwa sababu zilizoiletea Tanzania maendeleo tangu
ilipopata uhuru mwaka 1961.
Hayo
yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Spika Mstaafu, Pius Msekwa
wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii kuhusiana na hatua
ambazo Tanzania imepiga tangu ipate uhuru mwaka 1961.
Msekwa
alisema kuwa uongozi bora pamoja matumizi bora ya fedha ndizo nguzo kuu
zilizoiletea Tanzania maendeleo yanayoonekana leo ambapo takribani
sekta zote zimepiga hatua kubwa ukilinganisha na kipindi cha uhuru mwaka
1961.
“Wakati
tunapata uhuru mwaka 1961 tulirithi vitu vichache kutoka kwa wakoloni
ambavyo ni shule hospitali ya Muhimbili iliyokuwa ikijulikana kama
Princess Magreth ambayo kwa sasa imepiga hatua na kuweza kufanya
upasuaji wa moyo ambao haukuwahi kufanyika kwa miaka ya nyuma,”
alifafanua Msekwa.
Alisema
kuwa maendeleo yote hayo yametoka na juhudi za marais waliopita na
aliyepo, katika uongozi wao ambapo wamekuwa wakipambana na maadui watatu
wa maendeleo ambao ni ujinga, maradhi na umasikini.
Aidha
alisema kuwa viongozi hao wamekuwa wakipambana na maadui hao kulingana
na fedha ambazo zimekuwa zikipatikana katika kipindi cha uongozi wao.
Msekwa
aliwataka Watanzania kuendelea kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere kutokana na misingi aliyoiacha ambayo imeweza kutumiwa na
viongozi wa nchi na kuendelea kuleta maendeleo ambayo Tanzania
inajivunia hadi sasa.
0 comments:
Post a Comment