Na Nathaniel Limu-Singida
Wafanyabiashara
 wa kuku wa asili/kienyeji mkoani Singida wamejipatia mapato ya zaidi ya
 shilingi bilioni 1.8, baada ya kuuza kuku 151,242 katika kipindi cha 
mwaka jana hadi sasa.
Hayo
 yamesemwa juzi na kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji 
Beatus Choaji wakati akitoa taarifa ya uendelezaji wa kuku wa asili, 
kwenye kikao cha kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika kwenye 
ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa mjini 
hapa.
Chowaji amesema mapato hayo yamepatikana baada ya kuku hao 151,242 kusafirishwa  na kuuzwa nje ya mkoa ikiwemo jijini Dar-es-salaam.
“Kuku
 wa asili wakifungwa vizuri kwa kudhibiti ugonjwa wa mdondo na 
kuzingatia kanuni za ufugaji bora wanaweza kuleta mabadiliko makubwa na 
ya haraka ya kipato. Kuku wa asili pia ni lishe bora hususani kwa watoto
 na akina mama”, ameongeza Choaji.
Ili
 kuimarisha ufugaji kuku wa asili amesema imependekezwa halmashauri zote
 zitekeleze mkakati wa kuchanja kuku kwa wakati moja mara tatu kwa mwaka
 kwa kutumia watoa chanjo wasiokuwa wataalam wa mifugo.
Akisisitiza
 amesema “Mkakati huu unatarajiwa kuanza mara halmashauri 
zitakazokamilisha utoaji wa mafunzo kwa watoa chanjo hao. Halmashauri 
zimesisitizwa kushiriki kikamilifu kutekeleza mkakati huo ili kuinua 
kipato cha wananchi kwa haraka zaidi”.
Mapema
 Mkuu wa Mkoa wa Singida na mwenyekiti wa kikao hicho, Mhandisi Mathew 
John Mtigumwe, akifungua kikao hicho ameagiza kuwa wananchi 
wahamasishwe, ili wasiendelee kuuza chakula walichovuna msimu uliopita 
kiweze kuwafikisha msimu ujao wa mavuno.
Mhandisi
 Mitugumwe amesema kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) 
mvua za msimu huu zinatarajiwa kunyesha kwa kiwango cha chini ya 
wastani.
“Hivyo
 ni jukumu letu sote kuhimiza na kushauri wananchi kufuata kanuni bora 
za kilimo na kupanda mazo ya kipaumbele yanayostahimili ukame, na 
yanayokomaa mwa muda mfupi.
Wakati
 huo huo Mkuu huyo wa mkoa, ametumia fursa hiyo kutoa shukrani zake za 
dhati kwa wananchi wadau wa elimu, wafanyabiashara, kampuni za simu za 
viganjani na mashirika ya umma na binafsi, kwa kushiriki kutekeleza 
agizo la rais Magufuli la kumaliza uhaba wa madawati mashuleni.
0 comments:
Post a Comment