Wananchi
wa Kata ya Kitaraka iliyopo katika Halmashauri ya Itigi, Wilaya ya
Manyoni, Mkoani Singida, wamemuomba Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi, Mh. William Ole Nasha, kuwapatia shamba linalomilikiwa na
Serikali la Tanganyika Packers, ambalo Serikali imeacha kulitumia kwa
zaidi ya miaka 20, ili walitumie kwa shughuli za Kilimo na Ufugaji.
Wananchi
hao wamefikisha maombi hayo kwa Mh. Waziri alipotembelea shamba hilo
lenye ukubwa wa ekari 45,000, na kuzungumza na Wananchi wa Kata hiyo
waliolalamika kuwa hawana eneo la kulima wala kufuga ilihali shamba hilo
halitumiki na linafaa kwa shughuli hizo.
Nae
Mh. Waziri akizungumza na Wananchi hao amesema Serikali ya awamu ya
tano ni Serikali inayosikiliza kero za Wananchi na kuzishughulikia kwani
ipo karibu zaidi na Wananchi na ndio sababu ya yeye kufika Kijijini
hapo ili kuona namna bora ya kutatua changamoto hiyo na kuweka utaratibu
jinsi shamba hilo litakavyotumika.
"Wizara
inalichukua suala hili ikalitolee maamuzi, Wananchi wavute subira
wakingoja Serikali itoe ufafanuzi juu ya suala hili, ni marufuku
mwananchi yeyote kuvamia na kufanya shughuli za kilimo ama ufugaji kwa
sasa hadi hapo Serikali itakapotoa maelekezo mapya" alisema Mh. Nasha.
Mh.
Waziri pia akatoa wito kwa wafugaji wa maeneo hayo kuacha tabia ya
kukata miti hovyo, kwani kwa kufanya hivyo kwani wanaharibu mazingira na
watapelekea eneo lake kuwa jangwa, akawasisitiza kufuga ufugaji wa
kisasa kwa kufuga madume ya kisasa, kupunguza wingi wa mifugo ili
uendane na malisho waliyonayo, ukubwa wa eneo na kuendana na mabadiliko
ya tabia nchi, kuitumia mifugo yao kujiendeleza kiuchumi kama kuwasaidia
kujenga makazi bora na kushiriki kuchangia shughuli za maendeleo.
0 comments:
Post a Comment