Na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Dodoma
Maeneo
ya Kititimo na Kisaki mkoani Singida yametajwa kuwa ni miongoni mwa
maeneo mazuri nchini yenye uwezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya
upepo.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Medard Kalemani amesemwa hayo leo Bungeni
mjini Dodoma alipokuwa akijibu sawali la Mbunge wa Viti Maalum Jesca
Kishoa lililohoji ni lini mradi huo utaanza kuzalisha umeme huo mkoani
humo.
Akijibu
swali hilo Naibu Waziri Kalemani amesema Serikali kwa kushirikiana na
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imekuwa ikifanya tafti kwa ajili ya
kuzalisha umeme kwa kutumia upepo katika maeneo mbalimbali nchini.
“Ujenzi
wa mradi wa uzalishaji wa umeme wa upepo utaanza ifikapo Aprili 2017 na
kutarajiwa kukamilika mwaka 2019 baada ya majadiliano kati ya TANESCO
na kampuni ya Wind East Africa Ltd kukamilika mwezi Desemba 2016”
amesema Naibu Waziri Kalemani.
Kupitia
tafiti hizo, Naibu Waziri Kalemani amesema kuwa kampuni binafsi ya Wind
East Africa Ltd yenye Wabia watatu ambao ni Six Telecoms (Tanzania),
kampuni ya Kimataifa ya Aldwych ya nchini Uingereza pamoja na moja ya
wajumbe wa Benki ya Dunia (IFC) ambao utagharimu jumla ya kiasi cha Dola
za Kimarekani milioni 264.77.
Aidha,
Naibu Waziri Kalemani kampuni nyingine inayoonesha nia ya kuwekeza
katika mradi wa kufua umeme wa upepo ni mkoani Singida kuwa ni Geowind
Ltd ambayo ipo tayari kuzalisha umeme wa Megawati 50 eneo la Kititimo
ambapo kampuni hiyo tayari ina eneo la hekta 1,450, mradi huo
unatarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani milioni 136 na kukamilika mwaka
2018.
0 comments:
Post a Comment