Home » » "FANYENI KAZI KWA BIDII KWA MAENDELEO YA TAIFA" DAS PETER MASINDI

"FANYENI KAZI KWA BIDII KWA MAENDELEO YA TAIFA" DAS PETER MASINDI

Katibu Tawala wilaya ya Mkalama Ndugu Peter Masindi amewataka watumishi wilayani Mkalama kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidi katika kuwaenzi mashujaa wa nchi waliopigana kwa ajili ya taifa la Tanzania.
Kauli hiyo ametoa Julai 25, 2024 kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Mkalama wakati wa zoezi la usafi liliofanyika katika hosipitali ya wilaya ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Mashujaa nchini.
Serikali inaleta fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi, tuwajibike pamoja katika kuhakikisha fedha hizi zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Kila mmoja katika nafasi yake atimize wajibu wake, huwezi kuwa shujaa kama ukishindwa kutimiza wajibu wako, kwa kufanya hivi tutakuwa tumewaenzi Mashujaa wetu” DAS Masindi.
Katibu Tawala Peter Masindi amewasisitizia watumishi kuwahudumia wananchi kwa kutumia lugha nzuri pindi wanapokuwa wanatoa huduma kwa wananchi, kulinda maadili ya kazi pamoja na kudumisha amani na umoja baina yao “Tuache ubabe, tuache ufalme kwa kutumia ofisi zetu za serikali, bali tuwatumikie watanzania kwa lugha nzuri” DAS Masindi
Aidha Katibu Tawala Ndugu Peter Masindi amekumbusha watumishi na wananchi wilayani Mkalama kuhusu suala la kulinda maadili ya nchi yetu kwa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, vitendo vya ulawati na ushoga katika jamii zetu
“Ndugu zangu Tuhakikishe maadili ya watoto wetu yanajengwa na sisi wazazi, yanajengwa na sisi jamii iliyopo leo, tuhahitaji jamii yenye utuvuli , amani kwa ajili kufikia maendeleo ya taifa letu,hakikisha mtoto anaenda shule, huo ndio Ushujaa unaostahili” DAS Masindi

 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa