Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone(katikati) akifungua mkutano wa maelewano katia ya kampuni ya JEO na Wind East Africa, zinazotarajiwa kuzalisha umeme wa upepo katika manispaa ya Singida, viongozi wa NDC,Tanesco makao makuu na viongozi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Singida.Naibu waziri wa nishati na madini Mh. George Simbachewene (wa kwanza kushoto) ndiye aliyeitisha mkutano huo.Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Singida, Mwl.Queen Mlozi.
Mkurugenzi wa kampuni ya Wind East Africa, Rashidi Shamte akitoa nasaha zake kwenye mkutano huo wa maelewano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.
Afisa mwanadamizi wa shirika la Tanesco ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akitoa nasaha zake kwenye mkutano wa maelewano wa kampuni ya JEO na Wind East Africa.
Baadhi ya maafisa waandamizi wa kampuni ya Wind East Africa wakifuatilia kwa makini mkutano wa maelewano kati yao na wale wa JEO.
Baadhi wa viongozi wa shirika la Tanesco wakifuatilia kwa makini mazungumzo yaliyohusu maelewano kati ya kampuni ya Wind East Africa na JEO yanayotarajiwa kuanza kuzalisha umeme wa upepo katika manispaa ya Singida.
Naibu waziri wa nishati na madini Mh. George Simbachawene akihutubia wakazi wa kijiji cha Januka manispaa ya Singida.Mh. Simbachewene alifanya ziara katika kijiji hicho kukagua maendeleo ya mradi wa kufua umeme wa upepo.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Januka manispaa ya Singida wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na naibu waziri wa nishati na madini Mh. George Simbachawene (hayupo kwenye picha).Mkutano huo uliofanyika kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumzia mradi wa kufua umeme wa upepo kijijini hapo.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Makampuni mawili yanayotarajiwa kuzalisha umeme wa upepo katika manispaa ya Singida pamoja na kutoa ajira mbalimbali za kudumu yanatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 2,000 kwa wakazi wasiokuwa na taaluma ya aina yo yote.
Naibu waziri wa nishati na madini Mh. George Simbachawene, amesema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika katika kijiji cha Januka na Unyamikumbi ‘B’ manispaa ya Singida.
Amesema makampuni hayo ya Wind East Africa na JEO, licha ya kutoa fursa za ajira nyingi kwa wakazi wa manispaa ya Singida, pia uwepo wake utatoa fursa nyingi za kujiongezea kipato kwa wananchi.
Aidha, Mh. Simbachewene amesema umeme utakao zalishwa na makampuni hayo una ubora wa hali ya juu kuliko umeme wo wote unaozalishwa katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Awali kwenye mkutano wa pamoja kati ya makampuni hayo mawili, viongozi kutoka Tanesco Makao Makuu, NDC, na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Singida, Naibu waziri huyo ameyataka makampuni hayo yajiepushe na migongano ambayo haina tija kwao na nchi kwa ujumla.
Mh. Simbachewene amesema kuanzia sasa atakuwa nyuma ya mradi huo ili kuhakikisha mambo yanaenda vizuri na uzalishaji wa umeme unaanza kama inavyokusudiwa.
CHANZO MO BLOG