KAMPUNI
ya simu nchini (TTCL) mkoani Singida inadai zaidi ya shilingi
milioni 524.6 zikiwa ni malimbikizo ya ankra za matumizi ya simu kwa
wateja wake katika kipindi cha kuanzia mwaka juzi hadi machi
mwaka huu.
Meneja
biashara wa Kampuni hiyo ya TTCL mkoa wa Singida bw Mwindadi Baule,
amesema hayo wakati wa chakula cha mchana walichokiandaa kwa wafanyabiashara
wakubwa wa mjini Singida.
Lengo
la chakula hicho pamoja na kuimarisha mahusiano baina ya Kampuni na
wateja wake, ni kuwaelimisha wafanyabiashara hao kulipa madenbi yao kwa
wakati ili kuiwezesha Kampuni kujiendesha na kuboresha huduma.
Amesema
kutolipwa kwa wakati kwa deni hilo ni moja ya sababu
zinazoleta changamoto kubwa katika kuboresha huduma kwa wateja pamoja na
kusambaza zaidi huduma hiyo hadi Vijijini.
Hata
hivyo amesema mikakati mbalimbali imewekwa na kampuni hiyo ikiwemo
kutumia vyombo vya kisheria kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kila mteja
anayedaiwa analipa deni lake mara moja.
0 comments:
Post a Comment