SHULE ya Sekondari
ya Mwenge ya Mjini Singida ambayo hivi sasa inachukuwa
wanafunzi wa kidato cha tano na sita pekee, inadaiwa zaidi ya
shilingi milioni 396.6 na wazabuni waliofanya manunuzi na kutoa huduma
mbalimbali katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Mkuu wa Wilaya ya
Singida bibi Queen Mlozi amebainisha hayo jana wakati akitoa taarifa yake
kwa mkuu wa mkoa wa Singida Dokta Parseko Kone aliyefanya ziara ya kikazi ya
siku moja katika halmashauri ya Manispaa ya Singida ilipo shule hiyo
kongwe nchini.
Amesema kati ya fedha
hizo, shilingi milioni 357.6, ni madeni mbalimbali ya wazabuni waliotoa
chakula na huduma nyingine muhimu katika shule hiyo kwa kipindi cha
miaka kumi iliyopita.
Bibi Mlozi amesema kiasi
kingine cha zaidi ya shilingi milioni 38.9, ni madeni ya dawa na vifaa
mbalimbali vilivyotumika kufanyia majaribio maabara katika shule hiyo
tangu 2008 hadi mwaka jana.
Amesema deni hilo ni
kikwazo kikubwa kwa ustawi na maendeleo ya shule hiyo kutokana na
kushindwa kuamikika tena na wazabuni ili iendelee kupatiwa huduma mbalimbali.
Mkuu wa mkoa wa Singida
Dokta Parseko Kone ameahidi kuunganisha nguvu na mamlaka zingine
kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
0 comments:
Post a Comment