SHIRIKA lisilo la
Kiserikali la PSI-Tanzania kanda ya kati,limetoa msaada wa vitanda saba maalum
kwa ajili ya kujifungulia akina mama wajawazito kwa zahanati na vituo vya afya
saba mkoani Singida.
Msaada
huo wa vitanda vyenye jumla ya thamani ya zaidi ya
shilingi milioni sita , umezinufaisha Zahanati na vituo vya
afya vya Isanzu, Kinampanda, Zahanati na Hospitali ya Iambi
wilayani Mkalama pamoja na Sepuka, Tumaini na polisi katika halmashauri
ya wilaya ya Singida.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Mratibu wa afya ya uzazi wa PSI bibi Zena
Mgoi,amesema msaada huo umetolewa na shirika lao baada ya kubaini
mahitaji katika vituo hivyo vya tiba.
Bi
Zena amesema lengo ni kupunguza tatizo la vitendea kazi
katika hospitali, vituo vya afya na Zahanatiili kuhakikisha
kuwa wajawazito wanapata huduma bila matatizo yoyote wakati wa
kujifungua.
Viongozi
mbalimbali wa vituo vya tiba lvilivyonufaika na msaada
huo wametoa shukurani kwa shirika hilo na kuataka wadau wengine kuiga
mfano huo kwa kuchangia uboreshaji sehemu za tiba.
0 comments:
Post a Comment