Home » » Wauguzi Kilimatinde walia ukata

Wauguzi Kilimatinde walia ukata



index
Na Salesi Malula-Manyoni
 
Wauguzi wa Hospitai ya Kilimatinde wilayani Manyoni Mkoani Singida wako katika hali mbaya kifedha kutokana na kutolipwa mishahara yao kwa muda wa miezi mitatu ambapo hawajui hadi hivi sasa hatma yao itakuwaje.
Katika mahojiano maalum na Fullshangweblog timu ya wauguzi wanaofanyakazi kazi katika Hospitari hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Anglicana Dayosisi ya Bonde la Ufa wamesema wanasikitishwa sana na uongozi wa Hospitari hiyo kutowathamini na kuwacheleweshea mishahara huku baadhi ya madaktari wakiwa wamelipwa huku wauguzi tukiwa tunalia njaa kwani miezi mitatu ni mingi wanafikiri tutaishije? Alihoji mmoja wa wauguzi ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini kwa kulinda kibarua chake.
Wakieleza zaidi walisema kwakweli hali ni mbaya maisha ni magumu,na hatuna wa kumkimbilia kwani tuna taarifa kuwa baadhi ya Madaktari wenzetu wamelipwa lakini sisi hatuthaminiwi hii si sawa tunamuomba Mkuu wa wilaya ya Manyoni atusaidie tupate haki yetu aingilie kati suala hili kwani tunawakati mgumu sana kimaisha.
Mganga Mkuu wa Hospitari ya kilimatinde Dk. Tittus Uggu akiongea na mwandishi kupitia simu  yake ya Mkononi ya 0763…………… alikiri kuwa tatizo la kuchelewa kwa mishahara lipo na juhudi zinaendelea kwa ajili ya kulitatua kwani kulikua na tatizo la fedha hivyo amekiri pia baadhi ya madaktari kulipwa “niseme tu mwandishi kuna madaktari ambao malipo yao yanatoka serikalini hao wanalipwa moja kwa moja na kuna hao wauguzi ambao wako chini ya hospitari hawa tunawalipa kutokana na vyanzo vya mapato vya hospitalini na nakuhakikishia ndani ya siku hizi mbili au tatu wauguzi wote tutakua tumewalipa ila nikiri kuwa kweli tatizo hilo lipo”.
Habari za Jamii Blog

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa