Kamanda wa Polisi Mkoani Singida,SACP Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
WATU
watatu mkoani Singida wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwemo
la mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mng’imba Wilaya ya
Mkalama kusombwa na maji ya mto wa Ndurumo.
Kwa
Mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Singida,SACP Geofrey
Kamwela mwanafunzi huyo ni Mwajuma Jumanne mwenye umri wa miaka tisa.
Amesema
mwanafunzi huyo amesombwa na maji ya mto wa Ndurumo januari 28 mwaka
huu saa sita mchana wakati akivuka mto wa Ndurumo akitokea shuleni
akielekea nyumbani kwao.
“Mwili
wa mwanafunzi huyo ulionekana kesho yake saa nane mchana kandokando ya
mto Ndurumo katika eneo la kijiji cha Kidaru wilaya ya Iramba”,amesema
Kamwela.
Katika
tukio jingine,kamanda huyo alisema Ng’washi Gembuya (30) mkulima na
mkazi wa kijiji cha Mkiko wilaya ya Mkalama,alisombwa na maji ya mto huo
huo wa Ndurumo.
“Uchunguzi
wa awali wa jeshi la polisi,umebaini kuwa marehemu amefariki dunia
kutokana na kusombwa na maji yam to Ndurumo tangu januari 23 mwaka huu
saa 12.00 jioni wakati anajaribu kuvuka mto huo huku akiwa amelewa pombe
ya kienyeji”,alifafanua.
Wakati
huo huo,Kamwela amesema mtu ambaye hafahamiki anayekadiriwa kuwa na
umri kati ya miaka 25 na 30 wa jinsi ya kike,amefariki dunia kwa kuuawa
na watu wasiofahamika.
“Mwanamke
huyo alikutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa umechomwa moto na
kisha kutupwa kwenye daraja la kijiji cha Matipa manispaa ya
Singida.Polisi inaendelea na uchubguzi kujua sababu ya mauaji na watu
waliohusika”,amesema Kamanda Kamwela.
0 comments:
Post a Comment