Mkalama. Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, 
inatarajia kutumia zaidi ya Sh799.4 milioni kwa ajili ya miradi ya maji 
katika Vijiji vya Ng’ang’uli na Iguguno vilivyopo kwenye mpango wa 
Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Mradi wa Kijiji cha Ng’ang’uli, unatarajiwa 
kukamilika Januari mwakani, wakati ule wa Kijiji cha Iguguno utamalizika
 Aprili mwakani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Edward Ole Lenga wakati akizungumzia utekelezaji wa miradi hiyo.
Alisema miradi hiyo ambayo itanufaisha wakazi 
4,379 wa vijiji hivyo, ambapo mradi wa Ng’ang’uli ulianza Agosti mwaka 
jana na ule wa Kijiji cha Iguguno ulianza Septemba mwaka jana. “Hadi 
kufikia Novemba mwaka jana, utekelezaji wa mradi wa Ng’ang’uli ulikuwa 
umefikia aslimia 80 na ule wa Iguguno asilimia 30,” alisema Ole Lenga.
Aidha, alisema utaratibu wa kutumia mtaalamu 
mkandarasi wa nje umekuwa na matatizo mengi ya kiutawala ndani ya 
kampuni kiasi cha kusababisha baadhi ya miradi kuchelewa kukamilika.
“Utaratibu wa kutumia wataalamu washauri wa ndani,
 unaonekana kubadilisha sura ya utendaji kazi wa makandarasi. Ni muhimu 
kwamba usimamizi wa miradi ijayo utafanyika kwa utaratibu huu wa ndani,”
 alifafanua.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment