TAASISI ya
kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Singida, imepokea taarifa 102
za malalamiko dhidi ya vitendo vya kuomba na kupokea rushwa katika
kipindi cha kuanzia Januari hadi Disemba mwaka Jana.
Mkuu
wa taasisi hiyo mkoani Singida Joshua Msuya amesema hayo wakati akitoa taarifa
kwa vyombo vya habari, juu ya utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi cha
kuanzia Januari hadi disemba mwaka Jana.
Amesema
kati ya taarifa hizo, 87 ziko kwenye uchunguzi wa hatua mbali mbali, taarifa 13
zilitolewa ushauri kwa walalamikaji na taarifa mbili, zimehamishiwa katika
idara nyingine kwa hatua zaidi.
Akifafanua
zaidi, mkuu huyo,amesema kuwa taarifa hizo za mwaka jana, ni sawa na
ongezeko la asilimia 11.7 ikilinganisha na taarifa 94 za mwaka juzi
zilizofikishwa katika taasisi hiyo kuzuia rushwa.
Msuya
amesema ongezeko hilo linatokana na jitihada zilizofanywa na TAKUKURU mkoa za
kutoa elimu kwa wananchi na makundi mengine ya kijamii ili kuwajengea
ujasiri wa kufichua vitendo vya rushwa.
0 comments:
Post a Comment