Home »
» BASI LA SHABIBY LAPATA AJALI,28 WAJERUHIWA
BASI LA SHABIBY LAPATA AJALI,28 WAJERUHIWA
ABIRIA 28 wakiwemo
watoto wanne, wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Shabiby namba T
930 BUW, aina ya Utom, walilokuwa wakisafiria kugongana na lori la
mafuta na kupinduka katika Kijiji cha Kisaki.
Ajali hiyo imetokea
jana mchana umbali wakilomita 10 kutoka mkoani Singida kwenda Dodoma
wakati dereva wa basi hilo akijaribu kulipita lori upande wa kulia .
Lori
hilo lenye namba RAA 486N, aina ya Mercedes Benz, lilikuwa likitokea
Kigali, nchini Rwanda, kwenda Dar es Salaam likiendeshwa na Barimina
Benjamin (37).
Inadaiwa basi hilo lilikuwa na abiria 48 ambapo dereva
wake alikimbia baada ya ajali. Baadhi ya majeruhi waliozungumza na
Majira, walisema majeruhi wa ajali hiyo ni pamoja na kondakta Thadey
Mohando (34) .
Kondakta huyo anadaiwa kuvunjika miguu yote miwili na
mkaguzi wa basi William Hofini (39) alipata majeraha usoni na kwenye
mkono wa kulia .
Abiria wengine ambao walijeruhiwa walik imbizwa
Hospitali ya Mkoa huo kwa ajili ya matibabu ambapo Jeshi la Polisi
Kikosi cha Usalama Barabarani kilifika eneo la tukio kwa uchunguzi
zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa huo, Bi.
Queen Mlozi, aliwataka madereva kuzingatia sheria za Usalama Barabarani
ili kunusuru maisha ya watu.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ,
Dkt.Deogratius Banuba, alisema wamepokea majeruhi 28 wakiwemo watoto
wanne lakini wawili wa melazwa akiwemo kondakta wa basi na Agatha
Ally(20), mkazi wa Babati aliyeumia sehemu mbalimbali za mwili wake.
Chanzo:majira
0 comments:
Post a Comment