Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia afisa Wanyamapori katika halmashauri ya Wilaya ya Singida Augustino Lorry kwa tuhuma za kupatikana na silaha mbili na nyara za Serikali kinyume cha sheria.
Kamanda wa jeshi hilo mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi mwandamizi wa Polisi Geofrey Kamwela, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Jumatatu majira ya saa kumi na moja na nusu jioni nyumbani kwake akiwa na bunduki moja ya Rifle na nyingine Shot Gun na ndege 12 aina ya Flamingo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda Kamwela amesema siku ya tukio polisi walipata taarifa za siri kutoka kwa raia wema kuwa afisa huyo mwenye dhamana ya kulinda na kutunza maliasili za nchi anamiliki silaha kinyume cha sheria na kufanya biashara ya nyara za Serikali.
Amesema mbali na kumkamata afisa wanyamapori, pia wanamhoji mtu mwingine anayesadikiwa kuwa ni mshirika wake.
Hata hivyo amesema uchunguzi wa kina zaidi unaendelea kufanywa juu ya tukio hilo.
Kamanda Kamwela amesema kuwa watuhumiwa hao wanatarajiwa kupandishwa kizimbani wakati wowote kujibu shitaka la kupatikana na silaha za moto na nyara za Serikali kinyume cha sharia
Home »
» Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia afisa Wanyamapori katika halmashauri ya Wilaya ya Singida Augustino Lorry kwa tuhuma za kupatikana na silaha mbili na nyara za Serikali kinyume cha sheria.
0 comments:
Post a Comment