Meneja
wa SIDO mkoa wa Singida, Shoma Kibende akitoa nasaha zake muda mfupi
kabla hajatoa mikopo yenye thamani ya shilingi 18.9 kwa wajasiriamali wa
kikundi cha Urafiki cha mjini Singida.Kulia (aliyekaa) ni katibu wa
kikundi cha urafiki,Remiji Alex.
Meneja wa SIDO mkoa wa Singida,Shoma Kibenda,akimkabidhi Remji Alex mkopo wa shilingi 500,000.
Meneja
mikopo wa SIDO mkoa wa Singida, Ruben Mwanja akitoa mafunzo kwa
wajasiriamali muda mfupi kabla ya kukabidhi mikopo yenye thamani ya
zaidi ya shilingi 18.9 milioni kwa kikundi cha urafiki cha mjini
Singida.
Meneja
mikopo wa SIDO mkoa wa Singida, Ruben Mwanja (wa kwanza kulia) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wanakikundi cha wajasiriamali cha Urafiki cha
mjini Singida.Kikundi hicho kilikopeshwa zaidi ya shilingi 18.9 milioni
na watarudisha na fidia ya shilingi 1.8 kwa mwezi.(Picha na Gasper
Andrew).
Na Nathaniel Limu
MENEJA
mikopo wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) mkoa wa
Singida,Ruben Mwanja,amewataka wajasiriamali kutumia mikopo yao vizuri
na kwa malengo yaliyokusudiwa,na pia mikopo hiyo isaidie kuimarisha ndoa
zao.
Mwanja
aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi mikopo
mbalimbali yenye thamani ya shilingi 18,9 milioni kwa wanachama 39 wa
kikundi cha Urafiki cha Singida mjini.
Amesema
uzoefu unaonyesha wazi kwamba baadhi ya wanawake wanaobahatika kupata
mikopo,hukorofishanana au kutengana kabisa wanaume wao.
“Pia
wapo baadhi ya wanaume wakishapata mkopo wa kuendeleza biashara
yao,hukimbilia kuoa mke mwingine”,amesema Mwanja na kuongeza;
“Nawasihi
sana,mikopo ya SIDO isitumike kuongeza wake wengine au kuvunja ndoa za
watu,itumike tu kuendeleza biashara ya mkopaji ili kupanua/kuongeza
kipato cha mhusika”.
Kwa
upande wake meneja wa SIDO mkoa wa Singida,Shoma Kibenda,alikipongeza
kikundi cha Urafiki kwa madai kwamba kina utamaduni mzuri wa kurudisha
mikopo kwa wakati na bila matatizo.
Kibenda
aliwataka wapige hatua zaidi kwa kuangalia uwezekano wa kuanzisha
viwanda vidogo kama njia moja wapo ya kujiongezea kipato zaidi.
Mikopo
iliyotolewa juzi,kima cha chini kilikuwa shilingi 300,000 na cha
juu,kilikuwa ni shilingi 500,000 kwa mwanachama mmoja mmoja.Riba ya
mikopo hiyo ni asilimia 1.8 kwa mwezi.
0 comments:
Post a Comment