Mkuu
 wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone akizungumza kwenye uzinduzi 
wa mpango wa Tiba kwa kadi (TIKA) katika halmshauri ya manispaa ya 
Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aque Vitae Resort mjini
 Singida. Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi.
Meneja
 msaidizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Singida, Isaya 
Shekifu, akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa 
Singida.Dk.Parseko Kone, kuzindua mfuko wa Tiba kwa kadi (TIKA) katika 
manispaa ya Singida. Walioketi kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya 
Iramba,Yahaya Nawanda na Mstahiki Meya wa manispaa ya Singida,Sheikh 
Salumu Mahami.
Mkuu
 wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda, akitoa mada yake 
iliyohusu mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwenye mkutano wa wadau wa afya 
wa manispaa ya Singida.
Mkuu
 wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,(wa kwanza kulia) akisikiliza mada 
zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano wa wadau wa afya wa manispaa ya 
Singida. Wa kwanza kushoto,ni mstahiki meya wa manispaa ya 
Singida,Sheikh Mahami.
| Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na madiwani wa manispaa ya Singida.Walioketi wa kwanza kulia ni Diwani wa viti maalum Yagi Kiaratu na anayefuatia ni mstahiki Meya wa manispaa ya Singida,Sheikh Salum Mahami.Kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda na mkuu wa wilaya ya Iramba na Queen Mlozi, mkuu wa wilaya ya Singida.(Picha na Nathaniel Limu). | 
Na Nathaniel Limu, Singida
WADAU
 wa afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa kauli moja 
wameridhia kuanzishwa kwa Mpango wa Tiba kwa Kadi (TIKA) katika Manispaa
 hiyo.
Wadau
 hao wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa mpango wa TIKA una 
manufaa mengi ikiwemo mwananchi baada ya kulipa ada ya uanachama, 
atakuwa na haki ya kupata huduma za matibabu ndani ya Manispaa kwa mwaka
 mzima.
Kwa
 mujibu wa Meneja Msaidizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) 
Mkoani Singida, Isaya Shekifu mpango wa TIKA ambao unafafana na Mfuko wa
 Afya ya Jamii (CHF) unatumika mijini tu.
Shekifu amesema uanachama wa TIKA ni wa mtu mmoja mmoja, wakati ule wa CHF, ni wa familia au kikundi.
“Kwa
 sasa hapa Manispaa ya Singida, baada ya mpango huo kupata baraka ya 
kuanzishwa tunaendelea na mchakato wa kubadilisha sheria ndogo ya CHF 
kwenda kwenye Tiba kwa Kadi (TIKA)”,alifafanua Shekifu.
Meneja
 Msaidizi huyo amesema baada ya kukamilika kwa sheria ndogo 
itakayotawala uendeshaji wa TIKA, mpango huo utaanza rasmi mapema 
iwezekanavyo mwaka huu.
Akizindua
 mpango huo wa Tiba kwa Kadi (TIKA) katika Manispaa ya Singida juzi, 
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone amesema mpango wa TIKA 
utawahakikisha wakazi wa Manispaa ya Singida na viunga vyake mwanzo mpya
 wa kupata huduma za matibabu zenye uhakika.
Hata
 hivyo, Dk. Kone aliagiza viwango vya uchangiaji vya TIKA zitazingatia 
uwezo wa mwananchi kulipia pia vitazingatia hali ya sasa ya huduma za 
matibabu.
Katika
 hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa kuwa suala la TIKA ni la 
hiari wananchi watajiunga kwa wingi endapo watahamasishwa kikamilifu.
“Kila
 mmoja hapa awe balozi mzuri kwa kuhamasisha wannachi wajiunge na mpango
 huu mara baada ya sheria ndogo kupitishwa. Manispaa ihakikishe huduma 
zinakuwa bora katika vituo vyote ikiwa ni pamoja na lugha nzuri kwa 
wananchama”,amesema Dk.Kone
0 comments:
Post a Comment