Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone, amewataka 
wakazi wa Kanda ya Kati kutoa taarifa sahihi kwa wadadisi na wahariri wa
 utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi, ili Serikali iweze 
kutambua hali halisi ya ajira nchini. Dk Kone alitoa wito huo juzi 
wakati akifungua mafunzo ya wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu 
wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014. Alisema utafiti huo ambao 
mahojiano yake yanatarajiwa kufanywa katika kaya 11,520 nchini, 
unatarajiwa kuanza Februari mwaka huu na kwamba utatoa viashiria muhimu 
ikiwemo kujua hali ya ajira nchini.
Chanzo;Mwananchi 
0 comments:
Post a Comment