MATUMIZI mbegu bora na
pembejeo nyingine za kilimo pamoja na kuzingatia ushauri wa wataalamu,
vimetajwa kusaidia kuongeza mara dufu kiwango cha uzalishaji wa zao la alzeti
mkoani Singida.
Mtaalamu wa kilimo cha zao hilo
kutoka halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida bwana Elias Ziwa
amebainisha hayo katika taarifa yake juu ya mafanikio na changamoto
za kilimo cha Alizeti
Amesema kuwa uzalishaji alzeti
ambayo ndio zao kuu la biashara kwa wakazi wa mkoa huo, umeongezeka
kutoka magunia 4 kwa ekari miaka mitano iliyopita, hadi kufikia zaidi ya
gunia 12 hivi sasa.
Hata hivyo amesema pamoja na ongezeko hilo
amesema wameweka mkakati wa kuendelea kutoa elimu zaidi ili kufikia
hatua ya baadhi ya wakulima waliofanikiwa kuvuka kiwango hicho cha
uzalishaji alzeri kwa ekari gunia 15.
Kilimo cha alzeti ndio zao kuu la
biashara kwa wakazi wa mkoa wa Singida wapatao milioni moja na laki
tano, ambapo takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya tani 180,000 za zao hilo
huzalishwa kwa mwaka.
0 comments:
Post a Comment