HALMASHAURI ya wilaya ya Mkalama mkoani
Singida, inatarajia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 19 kutoka
kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato katika mwaka ujao wa
fedha wa 2014/2015.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Hassan
Mwachabuzi amebainisha hayo katika taarifa yake ya
mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha kwenye
kikao maalum cha baraza la madiwani.
Amesema wanatarajia kukusanya zaidi ya
shilingi milioni 600 kutoka vyanzo vyake vya ndani ya mapato, wakati Serikali
kuu itawapatia ruzuku ya shilingi milioni 360 kufidia vyanzo vya mapato
vilivyofutwa.
Amefafanua kuwa Serikali kuu
pia itatoa ruzuku ya zaidi ya shilingi bilioni 11.8 kwa ajili
ya mishahara ya watumishi wa halmashauri hiyo na ruzuku nyingine ya
zaidi ya shilingi bilioni 1.9 kwa matumizi yasiyo ya mishahara.
Mwachabuzi amesema Serikali kuu,
wafadhili, wahisani na wananchi, watachangia mapato ya zaidi ya shilingi
bilioni 4.6 bilioni, kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya
maendeleo katika jamii.
Hata hivyo pamoja na madiwani
kupitisha mapendekezo hayo ya bajeti, wamewataka watendaji
kuimarisha zaidi ukusanya mapato ya ndani na kubuni nyanzo
vingine badala ya kutegemea zaidi Serikali kuu na wafadhili.
0 comments:
Post a Comment