Mkuu
wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi, akizungumza kwenye ufunguzi wa
mafunzo ya wiki mbili ya wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye
uwezo wa kufanya kazi katika mikoa ya Singida ,Dodoma, Tabora na
Kigoma.Mafunzo hayo yanafanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa VETA mjini
Singida.
Baadhi
ya wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi
katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida na Dodoma wakiwa kwenye mafunzo
ya wiki mbili yanayohusu utafiti huo unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi
ujao.
Mkuu
wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya
pamoja na wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa
kufanya kazi katika mikoa ya Singida,Kigoma,Tabora na Dodoma na
wakufunzi wao.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU
wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone amewataka wakazi wa kanda ya kati
kutoa taarifa sahihi kwa wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye
uwezo wa kufanya kazi ili serikali iweze kutambua hali halisi ya ajira
nchini.
Dr.
Kone ametoa wito huo hivi karibuni wakati akifungua mafunzo ya wadadisi
na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka
2014.
Amesema
utafiti huo ambao mahojiano yake yanatarajiwa kufanywa katika kaya
11,520 nchini, unatarajiwa kuanza mapema mwezi ujao wa februari.
Dk.
Kone amesema utafiti huo wa nguvu kazi nchini, utatoa viashiria muhimu
ikiwemo kujua hali ya ajira nchini katika sekta rasmi na isiyo rasmi.
“Pia
utatusaidia kujua kiwango cha ukosefu wa ajira, kiwango cha ajira isiyo
timilifu, ajira mbaya, ajira hatarishi kwa watoto, hali ya kipato
kutokana na ajira, matumizi ya muda na ajira mpya zilizozalishwa katika
kipindi cha kuanzia mwaka 2006/ hadi 2013”,amesema.
Aidha
Mkuu huyo wa mkoa katika hotuba yake ilisomwa kwa niaba yake na DC wa
Singida, Queen Mlozi, amewahakikishia wananchi kwamba taarifa
watakazotoa zitakuwa ni za siri na zitatumika tu kwa matumizi ya
kitakwimu pekee.
Kutokana
na umuhimu wa utafiti huo, Dk. Kone amewahimiza wananchi wa mikoa ya
Singida, Dodoma, Tabora na Kigoma kutoa ushirkiano kama walivyoutoa
wakati wa zoezi la sense la watu na makazi agositi 2012.
Kwa
mujibu wa Dk. KOne jumla ya ajira 610,285 zimepatikana nchini
kutokanana uwekezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na
uwekezajikatika sekta binafsi kati ya mwaka 2010 hadi mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment