Baadhi
 ya wananchi wa Kijiji cha Zinziligi,tarafa ya Ndago,wilayani Iramba 
wakiwa kwenye viwanja vya mikutano ya Kijiji hicho wakipatiwa mafunzo na
 Kituo cha Msaada wa sharia kwa wanawake (WLAC) juu ya kutokomeza 
vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na ukeketaji pamoja na madhara 
yake.
Bi
 Esther Kileee (aliyemshikilia mkono ni Afisa mtendaji wa kata ya Ndago)
 kwanza    akitoa ushuhuda wa kuacha kujishughulisha na vitendo vya 
ukeketaji baada ya kuokoka na kwamba kabla ya kuokoka alikuwa akinufaika
 na shughuli hizo kwa kumpatia kipato chake na alaikuwa akiwakeketa 
wanawake wasiopungua 50 kwa mwezi.
  Mwanasheria
 wa WLAC,  Abia Richard akiwasilisha mada kwa wananchi wa Kijiji cha 
Zinziligi,Kata ya Ndago,wilayani Iramba ambapo pamoja na mambo mengine 
alisema katika kipindi cha wiki moja zaidi ya watu 1000 walipatiwa 
mafunzo na kati yao,wanafunzi ni 600 na watu wazima ni 500.
 Mwanasheria wa WLAC, Abia Richard ajiteta jambo na afisa mtendaji wa kata ya Ndago, Abeli Philipo Shaluo.
Igizo linaloashiria mwanaume anayemnyanyasa mkewe kwa kumfanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia.(Picha  zote Na Jumbe Ismailly)
Na Jumbe Ismailly- IRAMBA
KITUO
 cha Msaada wa sheria kwa Wanawake( WLAC) kimeanza kutoa mafunzo ya 
kutokomeza ukatili kwa kijinsia na ukeketaji pamoja na madhara yake kwa 
watoto wa shule za msingi za Nguvumali,Songambele na sekondari ya Ndago 
wilayani Iramba,Mkoani Singida ambapo katika kipindi cha wiki moja jumla
 ya wanafunzi 600 kutoka katika shule za msingi na sekondari walinufaika
 na mafunzo hayo.
Mwanasheria
 kutoka Kituo cha Msaada wa sheria na Wanawake (WLAC) Abia Richard 
aliyasema hayo kwenye mafunzo waliyotoa kwa wananchi wa Kijiji cha 
Zinziligi,Tarafa ya Ndago,wilayani Iramba.
Aidha
 Mwanasheria huyo wa WLAC alifafanua kwamba katika kipindi hicho cha 
wiki moja zaidi ya watu 1000 wameshapatiwa mafunzo hayo ambayo kati ya 
hao wanafunzi wa darasa la tano mpaka la saba wa shule za msingi na 
kidato cha kwanza hadi kidato cha nne ni 600 na watu wazima ni 500.
Akizungumzia
 sababu za kwenda kutoa mafunzo hayo kwa wanafunzi,Abia amezitaja kuwa  
ni kizazi na taifa la kesho,jambo ambalo endapo wakifahamu madhara yake 
mapema watakapokuwa wakubwa itakuwa rahisi kuepukananavyo.Kwa
 mujibu wa Abia kituo cha msaada wa sheria na Wanawake na watoto 
kikifadhiliwa na The Foundation For Civil Society kimekuwa kikiendesha 
mradi wake wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake pamoja na kuzuia 
vitendo vya ukeketaji kwa wanawake.
“Kwa
 hiyo tumefika katika wilaya ya Iramba,kata ya Ndago katika Kijiji cha 
Zinziligi kwa ajili ya kuongea na wanakijiji wa Zinziligi kujua ni aina 
gani ya ukatili wa kijinsia ambao unakumbana na wananchi wa Kijiji hicho
 pamoja na kupanga mkakati ni kwa namna gani wananchi hao wataepukana na
 ukatili huo”alisisitiza Mwanasheria huyo.
Kwa
 upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndago,Abeli Philipo Shalua 
alithibitisha kwamba asilimia 85 ya wanawake ndiyo wanaonyanyasika sana 
kwa waume zao na kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka jana mpaka sasa
 kuna matukio ya ukatili wa kijinsia 13 waliyofanyiwa wanawake.
Naye
 Mchungaji wa Kanisa la EAGT Zinziligi,Rejina Matoke huku akinukuu 
maandiko matakatifu aliweka bayana kuwa kitu kinachouwa nyumba za 
familia nyingi na kushindwa kuendelea ni tamaa ya uzinzi kwani hivi sasa
 suala la uzinzi limekamata watu wengi.“Zinziligi
 imekamatwa na uzinzi nasema ile kweli halafu kuna magonjwa ya kutisha 
hapa,hata kama leo daktari ataleta kipimo watakaopona ni wachache,idadi 
kubwa hapa ni taabu tu,watu hawajiheshimu”alisisitiza Mchungaji huyo.


0 comments:
Post a Comment