Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
29 January 2018
MADIWANI na Watumishi wa wa Manispaa ya Tabora wameagizwa kufuatilia makusanyo ya katika Stendi za Mabasi ya Tabora ili kujua mapato halisi yanayopatikana kila siku kwa ajili kudhibiti upotevu wa makusanyo katika stendi hiyo na kuiongezea Halmashauri hiyo makusanyo yake ya ndani.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Queen Mlozi wakati
akizungumza na Madiwani na Watumishi wakati wa kikao maalum cha kujadili
rasmi ya mpango wa bajeti ya mwaka ujao wa fedha.
Alisema
kuwa ni vema watembelea Stendi hiyo na kuangalia utaratibu unatumika
katika ukusanyaji mapato kutokana na magari yanapita na yale stendi hiyo
ili kujua fedha taslimu zinapatikana na kwa mwaka jambo
litakalowawezesha kujua Halmashauri inatakiwa ipate kiasi gani.
“Waheshimiwa
Madiwani nawaombeni sana muangalie upya makusanyo katika vyanzo vyenu
mbalimbali kama vile stendi na matangazo ili kujiridhisha kama
Halmashauri inachopata kinalingana na hali halisi au kuna mianya ya
upotevu ili tuizibe mapema” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Alisema
kuwa hatua itawasaidia kutekeleza maelekezo ya viongozi ikiwemo yale ya
Waziri Mkuu ya kutaka kila Halmashauri kuhakikisha inakusanya sio chini
ya 80 ya mapato yake ya ndani kila mwaka nje ya hapo viongozi
watawajibishwa.
Queen
aliongeza kuwa haipendezi kwa Halmashauri kama Tabora kujieleza kwa
kushindwa kufikia lengo wakati inaweza kubuni vyanzo mbalimbali ambavyo
vitawasaidia kuvuka lengo.
Alisema kuwa wanaweza kuanzisha eneo maaalumu kwa ajili ya wafanyabiashara (Machinga) kila mara moja kwa wiki ambalo linaweza kuwa chanzo kingine cha mapato.
Naye
Diwani wa Kata ya Ng’ambo George Mpepo aliwaomba Madiwani wenzake
kuufanyia kazi ushauri wa Mkuu huyo wa Wilaya kwa sababu utawasaidia
kuongeza makusanyo na kuwa na fedha kwa ajili ya kuwaletea maendeleo
wakazi wa Manisapaa ya Tabora.
Alisema
kuwa haipendezi kuona Halmashauri nyingine zinavuka lengo huko kila
mwaka inashindwa na kuongeza kuwa wakiendelea kushindwa ni vema Baraza
hilo la Madiwani livunjwe kwa kushindwa kutimiza majukumu yake.
“Mheshimiwa
Mkuu wa Wilaya ushauri wako umenigusa sana…naomba wenzangu
tukayazingatie hayo…na kama tutashindwa nitakuomba umuombe Waziri Mkuu
avunje Baraza hilo la Madiwani kwa kushindwa kusimamia shughuli
mbalimbali za maendeleo kuifanya Manispaa ya Tabora iendelee kuwa nyuma”
alisema Mpepo.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment