Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, ameonya kuwa watu watakaovuruga
mikutano ya kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Singida
Kaskazini, serikali itawashughulikia kwa mujibu wa sheria.
Dk.
Nchimbi alitoa onyo hilo katika Kijiji cha Mtinko Wilaya ya Singida
Vijijini alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu ya
tano kwenye uzinduzi wa kampeni hizo.
Alisisitiza
kwamba ili watambue kuwa ni mtumishi aliyetumwa na Chama Cha Mapinduzi
(CCM), ajitokeze mtu yeyote na kuthubutu kuvuruga ratiba ya mikutano ya
kampeni.
Hata
hivyo, aliwahakikishia wananchi kuwa mikutano ya kampeni itakuwa salama
pamoja na uchaguzi huo kwani serikali imejipanga kikamilifu kudhibiti
yeyote atakayeonekana anataka kuvuruga uchaguzi huo.
“Na
ole wake na atokee mtu yeyote yule mwingine atakaeingilia katika njia
hii ya uchaguzi salama, amani na utulivu ndipo mtakapotambua kwamba
nimetumwa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi,” alisema na kuongeza:
“Jiandaeni vizuri na wakati wa kura mjitokeze kwa wingi kupiga kura na kumchagua mgombea wa CCM, na siyo mwingine.”
Dk.Nchimbi
aliyataja baadhi ya mafanikio yaliyopo katika jimbo hilo ni bomba na
mafuta kutoka Horiri Uganda hadi Tanga ambalo kwa Singida Kaskazini lina
sifa ya pekee yake na litakuwa limenyanyuka kiuchumi kuliko sehemu
yeyote litakapopita.
“Na
hapa Singida Kaskazini kutajengwa kambi, patajengwa kituo watakuja
wataalamu na mabingwa wa hilo bomba ambao watakaa hapa kwa zaidi ya
miaka mia moja, hawatakaa pengine bali watakuja kukaa Singida
Kaskazini,”alisema.
0 comments:
Post a Comment