Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida, Thobias Sedoyeka akizungumza na
waandishi wa habari juu ya kupinga maandamano ya vyama vinavyounda
Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupinga matokeo ya tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) kumtangaza Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli.
Na Hillary Shoo, SINGIDA
JESHI
la polisi Mkoani Singida limepiga marufuku maandamano yanayotarajiwa
kuandaliwa na kufanyika chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ya
kupinga ushindi wa Rais Mteule John Magufuli katika Wilaya zote za Mkoa
huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi (ACP)
Thobias Sedoyeka alisema kuwa polisi wamepata taarifa za kiintelijensia
kuwa (kesho) leo kuwa vyama hivyo chini ya mwavuli wa UKAWA, viko katika
mipango ya chini kwa chini ili kufanya maandamano ya kupinga matokeo
hayo ya Urais.
“Uchunguzi
huo unaonesha kuwa maandamano hayo yatashirikisha makundi mbalimbali ya
watu hususan zaidi vijana na kupita sehemu mbalimbali za Miji kabla
ykuhitimishwa katika ofisi za CHADEMA Mkoa wa Singida.” Alisema Kamanda
Sedoyeka.
“Sisi
Jeshi la polisi Mkoani Singida tunasema kuwa maandamano hayo ni batili
na hatuyaruhusu kwa namna yoyote ili huku tukiwataka viongozi wa vyama
hivyo kutofanya hivyo kamwe na badala yake watumie njia stahiki za
utawala wa kisheria ikiwemo kwenda kwenye vyombo ambavyo vinawajibika
kushughulikia malalamiko yao.” Alisisitiza.
RPC Singida Thobias Sedoyeka.
Hata
hivyo alionya vijana kutojihusisha na maandamano hayo na badala yake
waendelee na kazi zao za uzalishaji mali kwani jeshi la polisi
halitasita kutumia nguvu za ziada pale itakapobidi kitendo ambacho
huenda kikaathiri utendaji kazi wao pamoja na watu wengine ambao
hawatahusika na maandamano hayo.
Hata
hivyo Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Singida, Shaban Limu alisema
walipeleka barua kwa OCD wa Wilaya zote za Mkoa wa Singida juu wa
kufanya maandamano hayo ya amani, lakini wamezuiwa kufanya hivyo na
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Singida.
Aidha
Limu alisema hivi sasa wanawasiliana na makao makuu ya CHADEMA, kupinga
amri hiyo ya Kamanda wa polisi Thobias Sedoyeka kwani kikatiba ni
halali kufanya maandamano bila kuvunja sheria za nchi, kwani kazi ya
polisi ni kuwalinda wakati wakiandamana.
Mwenyekiti
wa (Chama cha CHADEMA) Mkoa wa Singida, Shaban Limu akizungumza na
waandishi wa habari Mkoani Singida juu ya hatua yao ya kupinga amri ya
Kamanda wa polisi Mkoani humo Thobias Sedoyeka ya kuzuia maandamano yao
kupinga ushindi wa Dkt. John Magufuli .
Ofisi za CHADEMA Mkoa wa Singida (PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO).
Mo Blog
0 comments:
Post a Comment