Home » » 21 WAJERUHIWA WAKITOKA HARUSINI

21 WAJERUHIWA WAKITOKA HARUSINI

MTU mmoja amekufa na wengine 21 kujeruhiwa, baada ya basi dogo aina ya Coaster walilokuwa wakisafiria kutoka Shinyanga kwenye harusi, kurejea nyumbani kwao Morogoro kupinduka katika kijiji cha Ikugha wilayani Ikungi kwenye barabara kuu ya Singida - Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Queen Mlozi akizungumza kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, walikolazwa majeruhi, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 8.00 mchana.
Alisema kuwa ajali ilitokea baada ya Coaster hiyo, kuhamia upande wa kulia wa barabara, kukwepa uharibifu uliotokana na kungâ™oka mkanda wa chuma kwenye eneo hilo la daraja, hivyo kusababisha kugongwa kwa nyuma na basi la Zuberi lililokuwa likipita kwa kasi.
Jina la dereva wa basi hilo la Zuberi, lenye namba za usajili T 983 ABU, lililosababisha Coaster hiyo kupoteza mwelekeo na kupinduka mara tatu, halijafahamika.
Jina la aliyekufa kwenye ajali na majeruhi, hayakuweza kupatikana mara moja. Ajali hiyo imetokea kipindi ambacho kikosi cha usalama barabarani, kimeimarisha doria sehemu mbalimbali nchini.
Walioshuhudia ajali hiyo, walisema kuwa mwendo kasi na uzembe wa madereva, bado ni kikwazo kwa usalama barabarani.
Chanzo:Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa