CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimefanya mkutano mkubwa
na kujipatia wanachama wengi mahali panapodaiwa kuwa ngome ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) Singida Kaskazini, jimbo linaloongozwa na Waziri wa
Utalii na Maliasili Lazaro Nyalandu.
Katika mkutano huo uliofanyika juzi katika Kijiji cha Msange na
kuhutubiwa na naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zanzibar Salum Mwalimu,
ambapo zaidi ya wanachama 350 walikabidhiwa kadi pamoja na kuapishwa
kiapo cha uzalendo kwa ajili ya kuwajengea ujasiri.
Mwalimu aliwaambia wanachama hao kuwa kiapo hicho cha cha kuwajengea
ujasiri, ni kwa ajili ya kujiunga na kundi la watanzania wanaopigania
haki na matumaini ya taifa lao.
Alisema operesheni inayoendelea iliyopewa jina la Operesheni Delete
CCM (ODC) imelenga kuwafikia watanzania wote na kuwapatia ujumbe wa
namna sera na mikakati ya CCM ilivyoshindwa na kwamba kinastahili
kuondolewa madarakani kuanzia katika uchaguzi wa serikali za mitaa
unaotarajiwa kufanyika Disemba 14 mwaka huu na mkuu mwakani.
“Ndugu zangu nimefurahi leo (juzi) nimefika katika jimbo
linaloongozwa na Nyalandu ambaye ni mbunge wenu … nilikuwa natamani
kufika hapa ili nione mlivyo na maendeleo kwa kuwa mbunge wenu ni mtu
wa maraha nadhani anaweza kumshinda hata Rais Kikwete kwa kwenda nje
kufanya utalii” alisema Mwalimu na kuongeza
“Nilijua wenzetu kwa namna mbunge wenu alivyo, ninyi mtakuwa na
huduma bora za afya, elimu, barabara na maji kumbe hakuna kitu … lakini
sasa nadhani meonyesha kuondoa CCM, nafikiri hali kama mbunge wenu
ameiona, ni salamu tosha kwa chama chake kujiandaa na kufungasha virago
katika ofisi za serikali ifikapo mwakani.
Chanzo;Tanzania daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment