Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu ya mkono katika hospitali ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupata ajali ya lori iliyoua watu 6 katika kijiji cha Kijota Singida.
Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa huku akiendelea kupatiwa matibabu ya mkono katika hospitali ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupata ajali ya lori iliyoua watu 6 katika kijiji cha Kijota Singida.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa majeruhi wa ajali ya lori iliyoua watu sita wakiwa nje ya wodi za wagonjwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida.
Watu
sita wamefariki dunia huku wengine 42 wakijeruhiwa baada ya lori lenye
namba za usajili T.806 AEL aina ya scania mali ya Abdalla Mussa (39)
mfanyabiashara mkazi wa Mwenge mjini Singida, kuacha njia na kupinduka
katika Kijiji cha Kijota, Singida.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amesema ajali hiyo
imetokea Agosti 27 mwaka huu saa 1.30 usiku katika kijiji cha Kijota
wakati likitokea mnadani katika kijiji cha Mtinko Singida vijijini,
likielekea Singida mjini.
ACP
Magiligimba ametaja chanzo cha ajali kuwa ni uzembe wa dereva wa lori
hilo Jumanne Kidanka (32) Kamanda huyo amesema kuwa chanzo cha ajali
hiyo ni uzembe wa dereva ambaye hakuwa makini akiwa anaendesha lori hilo
lililosheheni abira na mizingo mingi.
Amewataja
waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Haji Jumanne (35), Mikidadi
Mohammed (40) wote wawili wakazi wa kijiji cha Mrama na Musa Salimu (30)
mkazi wa kijiji cha Mwakiti.
ACP
Magiligimba amewataja wengine kuwa ni Allen Mwangu (38) mkazi wa wilaya
ya Ikungi, Lucas Stephano (40) mkazi wa kijiji cha Mrama na Sharifa
Omari (19) mkazi wa kijiji cha Ilongero.
Ameongeza
kuwa majeruhi 20 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida, kumi
wamelazwa hospitali ya misheni ya Mtinko na wanne ambao hali zao ni
mbaya, wamelazwa katika hospitali ya misheni ya Hydom mkoani Manyara.
Ameeleza
kuwa baadhi ya majeruhi walipatiwa matibabu na kurejea makwao huku
wengine waliolazwa wamevunjika mikono, miguu na sehemu mbalimbali ya
miili yao.
“Hawa
wenye hali mbaya ni Fadhili Jumanne (33) mkazi wa Kibaoni mjini
Singida, Mikidadi Hamisi, Jafari Hamisi na Idrisa Ibrahimu, wote
wamevunjika miguu. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali
misheni Mtinko”, amesema.
0 comments:
Post a Comment