Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na wasimamizi wa miradi ya kutoa ajira za muda kwa wanufaika wa mpango wa Tasaf kutoka halmashauri na manispaa ya Singida wakati akifungua mafunzo ya uwezeshaji wa kusimamia miradi hiyo.
Wasimamizi wa miradi ya kutoa ajira za muda kwa wanufaika wa mpango wa Tasaf kutoka halmashauri na manispaa ya Singida wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya uwezeshaji wa kusimamia miradi hiyo.
Mratibu wa Tasaf Mkoa wa Singida Patrick Girigo Kasango akiwa na Afisa Ufuatiliaji kutoka Tasaf Sinith Haule wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uwezeshaji wa kusimamia miradi ya ajira za muda kwa wasimamizi wa kutoka halmashauri na manispaa ya Singida.
Wanufaika
wa mpango wa Kunusuru kaya masikini Tasaf, Mkoa wa Singida wametakiwa
kupanda mikorosho ili waweze kutunza mazingira pamoja na kujiongezea
kipato kutokana na zao la korosho.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa rai hiyo wakati akifungua
mafunzo ya uwezeshaji kwa wasimamizi 67 wa miradi ya kutoa ajira za muda
kwa wanufaika wa mpango wa Tasaf kutoka halmashauri na manispaa ya
Singida.
Dkt
Nchimbi amesema kutokana na kuwa ajira za muda kwa awamu hii zimelenga
katika utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti hivyo amewataka Tasaf mkoa
wa Singida kuwasiliana na Bodi ya Korosho waweze kupatiwa mbegu ili
isipandwe miti mingine bali mikorosho.
Amesema
kwa kufanya hivyo mkoa wa Singida utaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa
Korosho huku ajira hiyo ya muda ya kutunza mazingira kwa kupanda
mikorosho, ikiwa imewatengenezea wanufaika hao ajira yao ya kudumu.
“Tukiweza
kupanda mikorosho kwa zoezi hili la ajira za muda baada ya muda
wanufaika hawa wataweza kuwa na kipato kikubwa kwa kuweza kuuza korosho
zao, hii itakuwa ndio maana halisi ya mpango wa kunusuru kaya masikini
ambapo zinatakiwa pia zishiriki katika kukuza uchumi”, amesema na
kuongeza kuwa,
0 comments:
Post a Comment