Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Ni Mwenyekiti wa Bodi ya ESTL,Bi Rose Mjema akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya kupinga vitendo vya ukeketaji huku akitoa tahadhari juu ya madhara yatokanayo na vitendo hivyo vya ukeketaji.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).
Ni baadhi ya Mangariba na wakunga wa jadi kutoka katika Tarafa ya Mgori,wilayani Singida ambao wameamua kuachana na shughuli za kukeketa baada ya kupatiwa elimu na Shirika lisilokuwa la kiserikali la ESTL la Mkoani Singida,wakitoa ushuhuda kwenye uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukeketaji kwa wanawake katika Mkoa wa Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Singida.
Na Jumbe Ismailly SINGIDA
SHIRIKA
lisilokuwa la kiserikali la Empower Society Transform Lives (ESTL) la
Mkoani Singida limesema kwamba ukeketaji wa wanawake na watoto ni tatizo
kubwa Afrika,Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi 28 zinazotajwa
kuendeleza mila hiyo mbaya.
Hayo
yalisemwa na Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Mkoani Singida,Joshua Ntandu
kwenye risala aliyosoma wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutokomeza
ukeketaji katika vijiji 14 vilivyopo katika kata za Itaja,Mgori,Ntonge
na Ughandi,uliofadhiliwa na The Foundation For Civil Society na
kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Singida.
Aidha
Ntandu alifafanua kwamba inakadiriwa kuwa Tanzania ina zaidi ya
wanawake milioni 7.9 waliogundulika kuwa wamekeketwa huku Mkoa wa
Singida ukishika nafasi tano za juu za mikoa inayoongoza kwa ukeketaji
hapa nchini.
Alisema
tafiti zinaonyesha pia kwamba vitendo hivyo vinaendelea kuongezeka
katika Mkoa wa Singida na sababu kubwa zinazotajwa ni pamoja na imani
kwamba ukeketaji ni sehemu ya makuzi ya mtoto wa kike na kwamba humzuia
mtoto wa kike asiingie katika mahusiano ya mapenzi kabla ya kuolewa.Hata
hivyo Ntandu alisisitiza kuwa jamii pia huamini kwamba ukeketaji ni
tiba ya ugonjwa unaojulikana kama lawalawa kwa watoto wa kike (Vaginal
or Urinary Tract Infection (UTI).
“Kadhalika
kuna mbinu mpya ambayo imeshamiri ya ukeketaji wa watoto wachanga mara
tu wanapozaliwa na kabla ya kufikia umri wa mwaka mmoja,na hii hufanywa
ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria na vyombo vya dola”alisisitiza
Mtendaji mkuu huyo wa ESTL.
Akizindua
mradi huo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida,Afisa Ustawi wa
jamii wa Mkoa wa Singida,Shukurani Mbago,pamoja na kusikitishwa na
mbinu mpya iliyoshamiri ya ukeketaji wa watoto wachanga,alizitaja baadhi
ya sababu za kuongezeka kwa vitendo hivyo kuwa ni imani kuwa ukeketaji
ni sehemu ya makuzi ya mtoto wa kike na kwamba kumzuia mtoto wa kike
asiingie katika mahusiano ya mapenzi kabla ya ndoa.
“Jamii
pia huamini kuwa ukeketaji ni tiba ya ugonjwa ujulikanao kwa jina la
lawalawa kwa watoto wa kike mara tu wanapozaliwa na kabla ya kufikia
umri wa mwaka mmoja.”alifafanua Katibu tawala huyo wa Mkoa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ESTL Mkoa wa Singida,Rose Mjema
aliweka bayana kwamba mpaka sasa wameshaunda kamati za kutokomeza
ukeketaji katika ngazi za vijiji na kata kutokana na watu waliopo katika
ngazi hizo kuonyesha utayari wa kufanyakazi na wao.
Kwa
mujibu wa Mjema wajumbe waliopo katika kamati hizo ni ni vijana tu kwa
ngazi ya kata na vijiji,viongozi wa jadi,wakunga wa tiba asilia na
wakunga wa jadi kwa kuwaandalia vikundi vya kupiga vita masuala ya
ukeketaji kwenye maeneo yao.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Singida,Elia Digha akizungumza
na washiriki wa semina hiyo alishauri kwamba ili kukabiliana na vitendo
hivyo kuanzia ngazi za serikali za vijiji pamoja na Halmashauri waanze
kuandaa sheria ndogo itakayosimamia udhibiti wa ukeketaji katika
Halmashauri ya wilaya hiyo.
0 comments:
Post a Comment