Home » » UJUMBE WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WAENDELEA KUTEMBELEA MIGODI MIDOGO YA DHAHABU WILAYANI IKUNGI MKOANI SINGIDA

UJUMBE WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WAENDELEA KUTEMBELEA MIGODI MIDOGO YA DHAHABU WILAYANI IKUNGI MKOANI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Ujumbe kutoka Ofisi yaMakamu wa Rais ukiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji wakimsikiliza Mmiliki wa Mgodi wa Sambaru uliopo wilayani Ikungi Mkoani Singida, Bwana Yusuf Mwandami walipofanya ziara ya kutembelea mgodi huo.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,Bi Magdalena Mtenga akiuliza swali kwa mmiliki wa mgodi wa sambaru uliopo Ikungi Mkoani Singida mara baada ya ujumbe toka Ofisi ya Makamu wa Rais kutembelea mgodi huo wa mwisho katika picha ni Afisa madini kanda ya Singida aliyeongozana na ujumbe huo Bi. Sofia Omary.
Mmiliki wa Mgodi mdogo wa dhahabu wa Sambaru uliopo Ikungi Bwana Yusuf Mwandami akitoa maelekezo kwa ujumbe huo juu ya mashine mbalimbalimbali zilizofungwa mgodini hapo zitakavyokua zinafanya kazi. Wa kwanza kulia ni Afisa madini kanda ya Singida aliyeongozana na ujumbe huo Bi. Sofia Omary.
Ujumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa rais ukiongozwa na Mkurugenzi wa sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi-Mazingira Bi. Magdalena Mtenga wakipata maelezo juu ya uendeshaji wa mgodi mdogo wa dhahabu ulioko Ikungi Bwana Ahmed Magoma

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa