Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akisalimiana na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturumara baada ya kuwasili Mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua Miradi ya vyanzo vya maji.
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Ikungi mara baada ya kupita Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akielekea Manispaa ya Singida kwa ajili ya mapumziko, Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu
Baadhi ya Watumishi wa Wilaya ya Ikungi wakimsikiliza Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe mara baada ya kupita Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu (Kushoto) akimfatilia kwa makini Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe wakati wa kikao cha pamoja na watumishi wa Wilaya ya Ikungi, Mwingine ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Ndg Elieza
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Wilaya wakati wa ziara ya Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Na Mathias Canal,
Singida
Halmashauri ya
Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida imepongezwa kwa kuanzisha mpango mkakati wa
uundaji wa mamlaka ya maji katika makao makuu ya Wilaya ikiwa ni njia ya
utatuzi ya changamoto inayowakabili wananchi wengi ya upatikanaji wa maji kwa
wananchi.
Kauli hiyo
imetolewa na Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe wakati
akizungumza na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Ikungi walioongozwa na Mkuu wa
Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na kuhudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la
Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu.
Kauli hiyo inajili
wakati ambapo Naibu waziri Mhe Kamwelwe ameanza ziara ya kikazi Mkoani Singida
ambapo atatembelea na kukagua Miradi ya Maji na vyanzo vya uboreshaji
upatikanaji wa maji.
Alisema kuwa ili
kunusuru kadhia inayowakumba wananchi katika Wilaya hiyo ya uduni wa
upatikanaji wa maji ambapo wananchi wanaopata maji safi na salama ni 99,234
sawa na 32.2% ya wakazi wote 309,321 ni lazima kuwa na mbinu mbadala kupitia
wataalamu wa maji na ushirikiano mkubwa na Serikali katika Wizara ya Maji na
Umwagiliaji.
Mhe Kamwelwe alisema
kuwa Uongozi wa Wilaya ya Ikungi unatakiwa kupeleka mapema wizarani maombi ya uanzishaji
wa Mamlaka ya maji mji wa Ikungi ili timu ya wataalamu kutoka Wizarani iweze
kutumwa kwa ajili ya kujiridhisha.
Aidha, Alikiri
kuwa wingi wa watu Katika eneo la Ikungi unakidhi kuanzisha mamlaka ya maji mji
wa Ikungi kwani miongoni mwa sifa muhimu huwa ni pamoja na wingi wa watu.
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa hali ya upatikanaji wa
maji katika Wilaya ya Ikungi si wa kuridhisha sababu ambayo inapalekea wananchi
kwenda umbali mrefu na kutumia muda mwingi kupata huduma ya maji.
Alisema kuwa
pamoja na kuwa na matanki ya maji ya mvua ambayo mengi yamejengwa katika
taasisi za umma kama shule na vituo vya kutolea huduma za afya lakini bado
changamoto ni kubwa kutokana na kuwepo kwa kipindi kirefu cha kiangazi (Miezi
sita mpaka saba) na hivyo kufanya vyanzo vingi vya maji kutumika wakati wa
msimu pekee.
Mhe Mtaturu
alisema kuwa wakati wa kiangazi mifugo hupata maji kwenye malambo yaliyojengwa
kwenye vijiji vyenye miradi ya maji ya bomba, Mabwawa na Malambo au visima
walivyochimba wafugaji wenyewe.
Alisema pamoja na
kuwepo kwa Mabwawa na malambo kwa ajili ya kunyweshea mifugo na shughuli
zingine za binadamu katika sekta ya ujenzi na mahitaji ya majumbani lakini bado
Wananchi wanahitaji malambo zaidi ili kupunguza makali ya upatikanaji wa maji.
Kwa upande wake
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu Alishukuru kwa ajili
ya kupata fedha za kutengeneza miradi ya maji katika kata ya Sepuka, Kijiji cha
Nkhoiree Kata ya Iseke na Kijiji cha Tewa Kata ya Ntuntu.
Pamoja na Shukrani
hizo lakini pia Mhe Kingu alimuomba Naibu waziri huyo wa Maji na Umwagiliaji kusaidia
utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa kijiji cha Igilansoni
Kata ya Igilansoni kwani ni Kijiji kikubwa lakini kipo mbali na Vijiji vingine.
Hata hivyo katika
mwaka wa fedha 2017/2018 idara ya maji imepanga kuendelea kutoa huduma ya maji
safi na salama na upatikanaji wa maji ya kutosha kwa matumizi ya nyumbani na
kwa maendeleo ya shughuli za kiuchumi kwa kuongeza idadi wananchi wanaopata
maji safi na salama karibu na maeneo wanayoishi kwa kiwango cha 49% (June 2018).
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment