Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akishiriki zoezi la kutengeneza chaki katika kiwanda cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Miraji Jumanne Mtaturu akiwa amebeba ili kuzianika chaki alizotengeneza Mkoa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika kiwanda cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akikagua kiwanda cha kutengeneza jasi cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Dober Color wakifungasha chaki, Meneja wa Kiwanda hicho amesema sehemu ya kufungasha chaki hiyo inafanywa na wanawake kwakuwa wako makini na haraka.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amepiga marufuku Shule zote
Mkoani Singida kuagiza chaki nje ya Mkoa kwakuwa kuna viwanda
vinavyozalisha chaki bora mkoani hapa.
Dkt
Nchimbi ametoa katazo hilo mara baara ya kufanya ziara katika viwanda
viwili vinavyozalisha chaki katika halmashauri ya Itigi na kushuhudia
chaki yenye ubora ikiwa imezalishwa kwa wingi na ikiwa haijapata soko.
“Hawa
wenye viwanda wamejitahidi kuzalisha chaki bora haina vumbi na inauzwa
kwa bei sahihi lakini shule zetu badala ya kuja kununua hapa ambapo ni
karibu wanaagiza Dar es salaam na mikoa mingine”, amesema na kuongeza
kuwa,
“Yani
mnasubiri chaki hii hii iende Dar es Salaam halafu mnainunulia kutoka
huko, hii haikubaliki, kuanzia leo shule zote zinunue chaki hapa hapa
ili tupunguze gharama pamoja na kuinua viwanda vyetu”.Dkt
Nchimbi ameongeza kuwa Mikoa ya Jirani itakayonunua chaki katika
Viwanda vya Singida, vitasafirishiwa chaki hiyo bure kama motisha kwa
kuunga mkono viwanda hivyo.
Amezitaka
halmashauri kushirikiana katika kuboresha mazingira ya utendaji wa
viwanda hivyo hasa kwa kuangalia namna ya kuboresha barabara zinazoenda
katika machimbo ya jasi yanayotumika kutengeneza chaki kwakuwa wenye
viwanda wamekuwa wakilalamikia ubovu wa barabara hizo.
0 comments:
Post a Comment