Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji (wa tatu kulia) akikata
 utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa tawi la NMB Ikungi.
MKUU
 wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu ameyashauri mabenki 
ikiwemo NMB kubuni bidhaa zitakazowanufaisha Watanzania maskini ili 
kuondoa dhana inayowabaguzi ya kuwa "‘maskini sio rafiki wa taasisi za 
kifedha". Mtaturu ametoa wito huo juzi wakati akifungua rasmi Tawi la 
Benki ya NMB Ikungi. 
Alisema
 kuendelea kuamini kwamba maskini sio rafiki wa mabenki, kundi hilo la 
Watanzania litaendelea kudidimia ndani ya lindi la umaskini. “Kaeni 
muangalie kundi hili la watu maskini litanufaikaje na huduma 
zinazotolewa na mabenki ikiwemo ninyi NMB. 
Kundi
 hili la Watanzania maskini ili liweze kujikomboa kiuchumi, basi mabenki
 badala ya kutoa mikopo ya fedha taslimu, toeni mikopo ya mizinga ya 
nyuki, mabwawa ya kufungia samaki au kuku kwa ajili ya kufunga 
kibiashara”, alishauri Mtaturu. 
Akisisitiza,mkuu
 huyo wa wilaya, alisema ili Mtanzania akiwemo maskini aweze kupata 
maendekeo ya kweli ni lazima ajiongeze kwa kupata mikopo kutoka kwenye 
taasisi za kifedha. “NMB ninyi mnakwenda vizuri na mnakwenda na wakati. 
Mtaturu
 alisema sasa umefika wakati wa kuliangalia upya kundi la Watanzania 
maskini,ili na lenyewe liweze kushiriki kikamilifu kuipeleka Tanzania 
kwenye uchumi wa kati. Aidha, Mtaturu ametumia fursa hiyo kuwaalika 
wakazi wa wilaya ya Ikungi wahakikishe wananufaika kikamilifu na huduma 
mbalimbali zinazotolewa na tawi la NMB Ikungi.
 “Najua
 wazi wakazi wengi wa wilaya yetu wameshindwa kunufaika na huduma za 
kibenki ikiwemo mikopo, kutokana na benki zote kuwa Singida mjini umbali
 wa kilometa 45. Sasa NMB imesongeza huduma karibu, tuitumie fursa hii 
kwa kupata mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji na kupanua kilimo kikiwemo 
cha alizeti”, alisema. Katika hatua nyingine, mkuu huyo wa wilaya 
huyo,ametumia nafasi hiyo kuipongeza na kuishukuru benki ya NMB, kwa 
msaada wake wa vifaa tiba kwa kituo cha afya Ikungi vyenye thamani ya 
shilingi milioni tano.
 “Naagiza
 vitanda hivi vitatu vya kujifungulia, vifaa vya kujifungulia, vitanda 
na magodoro mawili ya kupumzikia wagonjwa na mizani mbili, vitunzwe 
vizuri viweze kutumika kwa kipindi kirefu”, alisema. Awali meneja NMB 
kanda ya kati, Straton Chilongola, alisema msaada huo wa vifaa tiba, ni 
mwendelezo wa NMB kuunga mkono serikali ya awamu ya tano katika 
kuboresha sekta ya afya. Alisema benki hiyo imeendelea kubuni bidhaa 
mbalimbali na zenye kuzingatia mahitaji halisi ya soko kwa wakati 
husika. 
“Moja
 ya bidhaa hizo ni kampeni ya ‘FANIKIWA’ akaunti ambayo ni mahususi 
kabisa kwa wajasiriamali wadogo wadogo.Wajasiriamali hao ni pamoja na 
baba/mama lishe, wauza chipis, wenye maduka ya biashara yakiwemo ya 
nguo”, alifafanua Chilongola. Akifafanua zaidi, alisema akaunti hiyo 
inampa fursa mteja kupata mkopo wa shilingi laki tano hadi shilingi 30 
milioni. Pia meneja huyo, alisema wanayo akaunti nyingine ya ‘Wajibu’ 
ambayo ni mahususi kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka 0-18. 
“Kwa
 upande wa teknolojia tuna akaunti ya ‘Chap Chap’. Akaunti hii mteja 
anaweza kufungua akaunti kwa muda mfupi na papo hapo kupata kadi yake ya
 ATM, na kuanza kufanya miamala wo wote”, alisema Chilongola. Benki ya 
NMB, ina matawi zaidi ya 200 na mashine za kutolea fedha zaidi ya 700 
nchi nzima. Ina wateja zaidi ya milioni mbili jambo linaloifanya kuwa 
benki pekee nchini yenye hazina ya wateja wengi kuliko benki zingine 
zilizopo nchini
0 comments:
Post a Comment