Mkurugenzi
wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali na
Mwenyekiti wa Mbao Fc Solly Zephania Njashi wakionyesha hati ya
makubaliano ya Mkataba ikiwa ni mkataba wa udhamini wa timu hiyo kwa
mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 140 sambamba na basi la wachezaji.
Mwenyekiti
wa Mbao Solly Zephania Njashi akizungumza na waandishi wa habari baada
ya kuingia makubaliano ya udhamini wa mkatabwa mwaka mmoja na na kampuni
ya GF Trucks & Equipments wenye thamani ya Milioni 140, kushoto ni
Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani
Karmali
Afisa
Masoko wa Kampuni ya GF Trucks & Equipments Kulwa Bundala
akizungumza na wanahabari baada ya kuingia mkataba na timu ya Mbao Fc
wenye thamani ya Milioni 140 kwa mwaka mmoja.
Mkurugenzi
wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali na
Mwenyekiti wa Mbao Solly Zephania Njashi wakionyesha jezi za Mbao
zitakazotumikia mwaka huu.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI
wa klabu ya Mbao Fc umeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya
milioni 149 na kampuni ya GF Trucks & Equipments ikiwa ni udhamini
wa timu hiyo kutoka Jijini Mwanza.
Kampuni
hiyo imeridhishwa na maendeleo ya timu hiyo na kuamua kuwapatia
udhamini kwani hawajawahi kushiriki katika udhamin i wa soka la Kiwango
cha ligi kuu.
Mkataba
huo uliosainiwa mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam,
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Imrani Karmali amesema kuwa mkataba
huo ni wa kihistoria kwani unaenda kuleta na kukuza maendeleo ya mpira
wa miguu nchini.
Karmal
amesema kuwa, madhumuni makubwa ni kukuza vipaji vya mpira wa miguu na
wanatarajiwa kuisaidia Mbao Fc kufikia malengo yao msimu huu, "
tunafahamu usafiri umekuwa ni tatizo kwa klabu nyingi ndogo za Ligi Kuu
na hicho kimetupelekea kuanza na basi msimu huu ambapo katika mkataba wa
milioni 140 utajumuisha sambamba na basi hilo la wachezaji lenye
thamani ya milioni 70,".
"uwezo
waliouonesha katika ligi kuu na hata kuingia fainali ya kombe la FA
ulituhamasisha kuifuatilia kwa ukaribu sana na tuna imani kwa msaada
wetu Mbao itaendelea kufanya vizuri na si hao tu bali hata ajira kwa
vijana zitaongezeka,"amesema Karmali.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Mbao Fc, Solly Zephania Njashi ameusifu mkataba
huo na kusema kuwa utazidi kuleta chachu ya maendeleo katika klabu yao
na hata kupunguza gharama za mahitaji kwa wachezaji.
Njashi
ameishukurui kampuni ya GF Trucks & Equipments kwa mkataba huo na
kuwaahidi mashabiki na wapenzi wa Mbao kuwa mwaka huu wataendelea
kufanya vizuri na kuendelea kusalia katika Ligi kuu msimu ujao.
Baada
ya kusaini mkataba huo, kampuni ya GF Trucks & Equipments i
iliwakabidhi mfano wa jezi zitakazovaliwa na timu ya Mbao tayari zikiwa
zimeshaweka nembo ya kamouni hiyo.
0 comments:
Post a Comment