Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jeshi
la Polisi Mkoani Singida, limefanikiwa kupunguza ajali za barabarani
kutoka ajali 69 kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi kufikia ajali 24 katika
kipindi cha mwezi Januari mpaka Juni mwaka huu.
Hayo
yamesemwa mwishoni mwa wiki na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Singida, ACP Debora Magilingimba wakati akitoa taarifa ya uhalifu kwa
Mkoa wa Singida ambapo amesema katika ajali hizo 24 zilisababisha vifo
vya watu 29 na hapajakuwepo majeruhi kabisa.
ACP
Magiligimba amesema kupungua kwa ajali kumetokana na Jeshi hilo kutoa
elimu ya usalama barabarani mara kwa mara hasa katika maeneo ya
vijijini, mitaani na hata katika mafunzo ya udereva.
Ameongeza
kuwa jeshi hilo limekuwa likithibiti mwendo kasi katika barabara kuu,
kuthibiti ulevi kwa upimaji wa kilevi kwa madereva wote wa vyombo vya
usafiri na hivyo kupelekea ajali kupungua sana kwa Mkoa wa Singida.
“Pia
tumeendelea kutoa elimu ya usalama barabarani mashuleni, vyuoni na
katika nyumba za ibada. Lengo ni kuiongozea jamii uelewa zaidi unaohusu
masuala yote ya ulinzi na usalama, na sheria za usalama barabarani”,
amefafanua.
Aidha,
ACP Magiligimba amesema makosa madogo yamepungua kwa asilimia 0.8
ambapo jumla ya makosa madogo 22,222 yameripotiwa katika kipindi cha
januari hadi juni mwaka huu, ikilinganishwa na makosa kama hayo 22,403
yaliyotokea kipindi kama hicho mwaka jana.
“Katika
makosa hayo madogo, jumla ya wakosaji 21,836 walilipa faini mbalimbali
zaidi ya shilingi milioni 655. Katika kipindi kama hicho mwaka jana
jumla ya wakosaji 21,778 walilipa faini mbalimbali zaidi ya shilingi
milioni 653.3. Faini hizo ni sawa na ongezeko la asilimia 0.3”, amesema
kamanda huyo.
ACP
Magiligimba ametaja baadhi ya mikakati mbalimbali ya
kukabiliana/kupunguza zaidi uhalifu, wahalifu na ajali za barabarani
kuwa ni kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kupitia vyombo vya
habari na kushirikiana na asasi mbalimbali katika kutoa elimu na
matengenezo ya barabara.
“Vile
vile tutaendelea kuimarisha ushirikiano zaidi na asasi zisizo za
kiserikali, ikiwemo World Future Vocation, mabalozi wa usalama
barabarani na SUMATRA. Pia tutashirikiana na TANROADS, halmashauri za
wilaya na manispaa kushauriana namna ya kufanya matengenezo ya barabara
katika maeneo yaliyoharibiwa au yenye kusababisha ajali za mara kwa
mara”, amesema ACP Magiligimba.
0 comments:
Post a Comment