Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Hivi
Karibuni, Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais Yoweri
Kaguta Museveni wa Uganda kwa pamoja waliweka jiwe la msingi la Ujenzi
wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga Tanzania.
Katika Makala hii pamoja na mambo mengine Mwandishi Said Ameir wa Idara
ya Habari- MAELEZO anaeleza kwani nini mradi huu ni kipimo cha utayari
na ujasiri wa watanzania katika kuchangamkia fursa.
Mradi
huu unaojulikana kama Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la
Afrika Mashariki (EACOP) unatekelezwa kwa ubia kati ya washirika wa
sekta binafsi na sekta za umma za nchi za Tanzania na Uganda.
Washirika
hao ni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya
Taifa ya Petroli ya Uganda (UNOC), Kampuni ya Mafuta ya Total ya
Ufaransa, Kampuni ya TULLOW yenye makao makuu yake London nchini
Uingereza na Kampuni ya China National Offshore Oil Company (CNOOC).
Bomba
ambalo litagharimu dola za kimarekani 3.5 bilioni, sehemu yake kubwa
yaani kilomita 1,115 kati ya kilomita 1,445 litajengwa katika ardhi ya
Tanzania na kupita mikoa 8, wilaya 24 na vijiji 184.
Kutokana
na hali hiyo, inaelezwa kuwa, mradi huu wakati wa ujenzi na
utakapokamilika, utatoa na fursa nyingi za kiuchumi ambazo zitasaidia
sana kuchangamsha shughuli za kiuchumi hivyo kuchangia ukuaji uchumi na
kuinua kiwango cha maisha ya watanzania kwa namna mbalimbali.
Mradi
huu ni mfano wa ushirikiano kati ya nchi za Tanzania na Uganda na kwa
upande mwingine ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na
sekta za umma katika nchi hizi.
Katika
hatua mbalimbali za utekelezaji wake, mradi huu utahitaji ushiriki wa
sekta binafsi katika nchi zote mbili na wakati mwingine hata taasisi
nyingine za umma ambazo zinatoa huduma zitakazohitajika na mradi.
Kwa
hiyo, wakati tukisifia kuwa ni mfano wa mradi wa ubia wa sekta ya umma
na sekta binafsi katika nchi zetu, watanzania hawana budi kuelewa kuwa
wana wajibu mkubwa wa kuzitumia vyema fursa za mradi huu.
Kwa
Tanzania, mradi huu unaweza kuonesha picha halisi ya ushirikiano wa
sekta hizo kwa kuzingatia namna makampuni na taasisi za humu nchini
zitakavyoweza kushiriki na kufanikisha mradi huu.
Kwa
maana nyingie ni mradi ambao unaweza kutumika kupima utayari, umakini,
uwezo na ujasiri wa watanzania katika kuchangamkia fursa za kiuchumi.
Kama
alivyoeleza Rais Magufuli wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la
msingi kuwa katika mradi huu, Serikali imesamehe mambo mengi ili uweze
kutekelezwa kwa kuishirikisha Tanzania. Wataalamu wa nchi walichambua na
kupembua hadi kubaini kuwa kusamehe huko kutafidiwa na fursa nyingi
zitakazoletwa na mradi huu.
Kwa
maana hiyo bila ya watanzania kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha
wanazitumia kadri itakavyowezekana fursa hizo uamuzi huo wa Serikali
kusamehe hivyo ilivyovisamehe hautakuwa na maana yeyote.
Kuja
kwa mradi huu Tanzania, watanzania hawana budi kuipongeza Serikali
chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa jitihada kubwa kwa kutumia
ushawishi wa kisiasa, kidiplomasia, uchumi na ukaribu wa viongozi wa
nchi hizo mbili pamoja na hoja nyingine hadi kufanikisha mradi huu kuja
Tanzania.
Jitihada
hizi ni kielelezo cha dhamira ya kweli iliyonayo Serikali ya Awamu ya
Tano ya kutafuta kila aina ya fursa za kiuchumi ambazo zitasaidia
kutimiza ahadi zake kwa watanzania ya kujenga Tanzania yenye uchumi
imara.
Serikali
imejitwika mzigo mkubwa wa kushiriki katika kutekeleza mradi huu mkubwa
wa aina yake lakini imefanya hivyo kwa kuamini kuwa watanzania wako
tayari na wako imara kuupokea kwa hali na mali.
Imeelezwa
mara kwa mara kuwa mradi huu utaliingizia taifa mapato makubwa, utaleta
tekinolojia na utalaamu na fursa za kiuchumi ambazo watekelezaji wake
kwa kiwango kikubwa ni kutoka sekta binafsi. Kwa mnasaba huo, Serikali
hapa imefanya zaidi ya wajibu wake ambao ni wa kujenga mazingira mazuri
ya kuvutia uwekezaji.
Wale
wahenga wa Cambrigde walisema“give us the tools and lets finish the
job” na hivi ndivyo ilivyofanya Serikali kwa mradi huu. Imeleta mradi na
kufungua fursa tele ambazo watanzania wanapaswa kuzitumia kujenga
kiuchumi wao binafsi na uchumi wa taifa.
Haitakuwa
na maana hata kidogo katika ngazi ya serikali na katika ngazi ya
Mtanzania mmoja mmoja kufika wakati fursa za mradi huu kuchukuliwa na
wageni kwa sababu zozote na katika mazingira yeyote yale. Ikifikia hatua
hiyo watanzania watakuwa wamewaangusha viongozi wao.
Hii
kutokana na mazingira ambayo Serikali imeyaweka kuwawezesha watanzania
kushiriki katika sekta ya mafuta na gesi asilia. Mbali ya kupitisha
Sheria ya Local Content Act ya 2015 ambayo inasisitiza ushiriki wa
watanzania lakini zaidi dhamira ya kweli ya kisiasa iliyonayo uongozi wa
Serikali ya kuhakikisha kuwa watanzania wanafaidika ipasavyo na mradi
huu.
Ni
jambo la kutia moyo kuona kuwa baadhi ya Taasisi za Serikali na za
sekta binafsi zimeshaanza maandalizi au zimejitokeza kuwaandaa
watanzania kuchangamkia fursa hizo na kuhakikisha wanazitumia vyema.
Miongoni
mwa taasisi hizo ni Jumuiya ya Watoa Huduma katika Sekta ya Mafuta na
Gesi (ATOGS) ambayo inawakusanya pamoja watoa huduma katika sekta hiyo
ambapo lengo lake kubwa ni kuhakikisha kuwa fursa za mradi huo
zinatumika ipasavyo kwa manufaa ya muda mfupo na mrefu ya watanzania.
ATOGS,
kama taasisi nyingine zitakazoelezwa baadae, imeonesha mfano wa utayari
kwa kuwa na mpango mkakati wake ambao unalenga kuwawezesha watoa huduma
wa humu nchini wanapata fursa hizo kwa kuwasaidia kwa namna mbali mbali
tangu hatua za awali za kuwania fursa hizo hadi utekelezaji wake.
Makamu
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Abdulsamad Abdulrahim katika moja ya
mikutano na waandishi wa habari alisema taasisi yake imejipanga
kuwajengea uwezo watoa huduma na kutoa wito watoa huduma hao kwa
waliokuwa bado hawajajiunga wajiunge na taasisi hii kwa minajili ya
kufaidika na uwezeshaji wao.
Halikadhalika,
Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) nalo linaeleza kuwa
limejidhatiti kuhakikisha kuwa watanzania watakaobahatika kupata fursa
za kutoa huduma katika mradi huo hawashindwi kwa kukosa fedha za
kutekeleza kandarasi zao.
“Hatutaki
kusikia mtanzania amekosa fursa hii kwa sababu ya kukosa fedha
…ukibahatika njoo kwenye Baraza tutakushauri… Serikali ina mifuko 17
yenye fedha za kutosha kukuwezesha” anaeleza Mkurugnezi wa uwezeshaji wa
NEEC Bwana Edwin Chrisant.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini
(TPSF) Bwana Godfrey Simbeye aliwaambia waandishi wa habari kuwa taasisi
yake imejipanga kuhakikisha kuwa mikataba ya kandarasi itakayofikiwa
inazingatia maslahi ya pande zote na utekelezaji wake unafanyika
kulingana na vipengele vya mikataba.
Dhamira
hizi zilizoelezwa na taasisi hizi muhimu nchini, hapana shaka yoyote
kuwa ni habari njema inayoashiria matumaini makubwa na kuonesha sasa
watanzania wameamka na wamedhamiria kujenga Tanzania mpya kwa kila mmoja
kwa nafasi yake kuyatumia mazingira yaliyopo kujenga uchumi wa taifa.
Kama
kweli taasisi hizi zitatekeleza yale ziliyojipangia ikiwemo kuwapatia
watoa huduma msaada wa kitaalamu, huduma za kisheria, kifedha, viwango
na vigezo katika manunuzi, utaalamu, kuwaunganisha na wabia, kuwajengea
uwezo vijana wasomi ili waweze kushika nafasi zitakuwa zimetoa msaada
mkubwa kwa nchi.
Kwa
hakika mradi huu kama ilivyoelezwa awali utakuwa kigezo muhimu kupima
utayari, umakini na uwezo wa sekta binafsi kuchangamkia fursa
zinapotokea na mafanikio ya ushiriki wa sekta hiyo huenda ukawa mwanzo
mzuri wa kuupa mgongo utamaduni ulizoeleka wa watanzania kulalamika
hususan kuilalamikia Serikali kuwa haiwapi fursa kama hizi.
Wahenga
walisema “shike shike na mwenyewe nyuma” kwa hili Serikali zimefanya
wajibu wake sasa mpira uko kwa wadau katika sekta binafsi kuucheza kwa
zitumia fursa na ni vyema kukumbuka kuwa “mso matendo hula uvundo” hivyo
watanzania wachangamkie fursa wasije wakajikuta karamu imekwisha
‘wakaramba vyungu.
Ni
vyema pia kutanabahisha kuwa fursa za mradi huu haziko kwa watoa huduma
kama hao pekee ambao wao ni wafanyabiashara na wataalamu ambao tayari
wanajielewa, wana uwezo na wako katika sekta hiyo hivyo tunaweza kusema
wana angalau uzoefu.
Lakini
ukweli hi kuwa fursa za mradi huu zimetapakaa kila mahala katika ngazi
mbali mbali kuanzia wakulima wa jembe la mkono, wafugaji wadogo wadogo,
mafundi mchundo, hadi vibarua wa ujenzi. Hivyo taasisi zinazohusika
zinapaswa pia kuliangalia kundi hili kubwa na kuhakikisha linashiriki
vyema.
Hii
ni kwa sababu, inapozungumziwa ajira elfu kumi na ajira nyingine zaidi
ya elfu thelathini nyingi zinawagusa watanzania wa kundi hili. Ikumbukwe
kuwa kundi hili ambalo ndilo litakalokuwa karibu na mradi ndilo
litakalokuwa la kwanza kulalamika pindi litakapokosa fursa na kujikuta
halina namna ya kushiriki na kufaidika.
Utekelezaji
mzuri na wenye ufanisi wa mradi huu kwa kushirikisha sekta binafsi
nchini utakuwa kigezo cha kufungua milango kwa miradi mingine mikubwa ya
aina hii humu nchini.
Watanzania hawana budi kumpongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kujenga Tanzania Mpya yenye matumaini mapya. Hakika Tanzania yenye uchumi wa kati na ya viwanda inawezekana, kama kila mmoja atatimiza wajibu wake
0 comments:
Post a Comment