Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkazi
wa kijiji cha Shiponga, Hanang Mkoani Manyara anayedaiwa kuwa jambazi,
Hamisi Athumani (32), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kiunoni na
askari polisi wakati akiwa katika harakati ya kutoroka.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa, ACP Debora Magiligimba, amesema tukio
hilo limetokea Agosti 25 mwaka huu saa nane mchana, huko katika kijiji
cha Mgori tarafa ya Ngimu wilaya ya Singida.
Amefafanua
kuwa Hamisi (marehemu) alipigwa risasi na askari polisi wakati
akijaribu kuwatoroka mara baada kuonyesha bunduki aina ya rifle yenye
namba 7358 na risasi zake tano.
Amesema
bunduki hiyo iliyokuwa imekatwa mtutu na risasi zake tano zilikuwa
zimefichwa kwenye soksi, vitu hivyo vilikuwa vilihifadhiwa kwenye mfuko
wa sandarusi, na kufichwa chini ya jiwe.
ACP
Magiligimba amesema Agosti 23 mwaka huu, mtuhumiwa alikamatwa na
wananchi wa kijiji cha Ngamu, na kufikishwa katika kituo cha polisi cha
kijiji hicho kwa tuhuma ya kujihusisha na matukio ya ujambazi.
“Kesho
yake mtuhumiwa alihojiwa na kukiri kujihusisha na matukio ya ujambazi
wa kutumia silaha katika mikoa mbalimbali. Pia aliahidi kuwapeleka
askari kuwaonyesha mahali alikoificha silaha anayoitumia kwenye matukio
hayo ya ujambazi,” amesema ACP Magiligimba.
Kamanda
huyo amesema Agosti 25 mwaka huu saa sita mchana, askari polisi wakiwa
na mtuhumiwa, walikwenda katika pori la kijiji cha Mgori mahali
alipokuwa ameficha bunduki hiyo aina ya rifle.
“Mara tu baada ya kuwaonyesha askari hao silaha hiyo na wakati askari wanaendelea kufanya upekuzi katika eneo hilo, mtuhumiwa alijaribu kutoroka askari kwa kukimbia” amesema na kuongeza.
“Askari
mmoja alifyatua risasi tatu hewani akimtaka asimame, lakini hakutii.
Ndipo alipompiga risasi moja iliyompata sehemu ya kiunoni”.
Amesema
jereha hilo la risasi lilisababisha mtuhumiwa Hamisi avuje damu nyingi,
na hivyo kufariki dunia wakati akikimbizwa hospitali ya mkoa kwa
matibabu.
“Jeshi
la Polisi Mkoa wa Singida linaendelea kutoa wito kwa wananchi waote
kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini wahalifu katika maeneo yao ili
hatua ziweze kuchukuliwa kudhibiti vitendo vya kihalifu,” amesema kamanda huyo.
0 comments:
Post a Comment