Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mkuu
 wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Eng. Jackson Makata (mwenye 
miwani) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi la Benki ya NMB 
Mkalama. Wengine ni maofisa wa NMB na
wageni waalikwa wakishuhudia tukio hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Eng.Jackson Makata akizindua rasmi tawi la NMB wilayani humo.

Mkuu
 wa Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Eng. Jackson Makata (mwenye 
miwani) pamoja na maofisa wa NMB wakifurahia mara baada ya kukata utepe 
kuashiria uzinduzi wa Tawi la
Benki ya NMB Mkalama.
MKUU wa
 Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Eng. Jackson Jonasi Masaka, 
amewaagiza
madereva wa boda boda kuanzisha na kusajili vikundi vya ujasiriamali, 
ili kujijengea mazingira mazuri kupata mikopo toka tawi la NMB benki, 
lililozinduliwa wilayani humo. Eng. Masaka ametoa agizo hilo juzi wakati
 akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa tawi la
NMB tawi la Mkalama, lililopo katika makao makuu ya wilaya hiyo, 
Nduguti.
Alisema
 kufunguliwa kwa tawi hilo kumesogeza karibu zaidi huduma mbalimbali 
ikiwemo ya
mikopo zinazotolewa na NMB benki, kwa wakazi wa wilaya hiyo. Akifafanua,
 alisema huko nyuma wakazi wa wilaya hiyo pamoja na watumishi wa umma, 
iliwabidi kufuata huduma za kibenki Singida mjini, umbali wa kilometa 
140 kwenda na kurundi.
“Kwa
 hiyo ninyi madereva wa bodaboda, NMB imesongeza huduma...huu ni wakati 
muafaka kuboresha
shughuli zenu. Msilale changamkeni, jiungeni kwenye vikundi 
vilivyosajiliwa muweze kupata mikopo itakayokuza mitaji yenu. Mjue tu 
kwamba dereva mmoja mmoja ni ngumu mno kupata mkopo kwenye taasisi za 
kifedha”, alisema mkuu huyo wa wilaya. Eng. Makata pia ametumia
fursa hiyo kuwahamasisha baba/mama lishe, wauza chips na wajasiriamali 
mbalimbali wakiwemo wadogo, kuchangamkia mikopo kupitia akaunti ya 
‘FANIKIWA’.
“Niipongeze
 NMB benki kwa kubuni bidhaa hii ya akaunti ya FANIKIWA. Kupitia akaunti
 hii
ya FANIKIWA, wajasiriamali niliowataja hapo juu, wataweza kupata mikopo 
kati ya shilingi laki tano na milioni 30. Nasisitiza tumieni fursa hizi 
zilizosongewa karibu zaidi na NMB, ili mkuze mitaji yenu iweze kukidhi 
mahitaji ya wakati wa sasa,” alisema.
Katika
 hatua nyingine, mkuu huyo wa wilaya ameishukru na kuipongeza NMB benki 
kwa msaada
wake wa vitanda 15, magodoro 15, vitanda viwili vya kujifungulia akina 
mama wajawazito na mashine mbili za kupimia mapigo ya moyo.
“Msaada
 huu wenye thamani ya shilingi milioni 10 ambao umetolewa kwa kituo cha 
afya, vitunzwe
na kulindwa vizuri ili viweze kutumika kwa kipindi kirefu,” alisema Eng.
 Makata. Awali meneja wa uhusiano wa biashara kati ya serikali na benki 
NMB kanda ya kati, Yasin Mfinanga, alisema msaada huo ni mwendelezo wa 
NMB katika kumuunga mkono Rais Dk. Magufuki
kuboresha sekta ya afya.
“Kila
 mwaka baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji, benki yetu huwa 
inatenga asilimia
moja ya faida, kwa ajili ya kutoa misaada inayolenga sekta ya afya na 
elimu. Agizo la rais Magufuli la kuchangia madawati katika shule za 
msingi na sekondari, NMB ilishiriki kikamilifu,” alisema Mfinanga kwa 
kujiamini.
Mfinanga
 alitumia fursa hiyo kuwataka wakazi wa kanda ya kati, kuacha kabisa 
utamaduni
wa kutunza fedha kwenye simu zao za viganjani na badala yake wazitunze 
kwenye mabenki ikiwemo ya NMB. Akisisitiza, alisema fedha zinazotunzwa 
kwenye simu za viganjani usalama wake ni mdogo mno, ikilinanishwa na 
zile zinazotunzwa kwenye mabenki ya kuaminika.
“Fedha
 hizi zilizopo kwenye simu za viganjani na wakazi wa kanda ya kati 
wakijitokeza
kwa wingi kuweka fedha benki, hatua hiyo itachangia NMB benki kuwa na 
uwezo mkubwa katika kutoa mikopo. Aidha, hatua hii itachangia benki 
kupunguza riba zinazokatwa kwenye gharama za uendeshaji,” amesisitiza 
zaidi.
Wakati
 huo huo.mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama, James Mkwega, 
alisema kufunguliwa
kwa tawi la NMB tawi la Mkalama, pamoja na mambo mengine, kutachochea 
ukuaji wa uchumi. “Binafsi nimefarijika mno…na naipongeza NMB benki 
kufungua tawi hapa kwetu Nduguti makao makuu ya wilaya ya Mkalama. Huko 
nyuma tulilazimika kufuata huduma za kibenki Singida
mjini kilometa 140 kwenda na kurudi. Madhara yake yalikuwa makubwa mno,”
 alisema na kuongeza;
“Watumishi
 wa umma wakiwemo walimu nao wametaabika sana katika kufuata mishahara 
yao New
Kiomboi wilaya ya Iramba umbali wa likometa 90. Hapo ilikuwa kabla 
wilaya Iramba yaijagawanywa na kuzaa wilaya ya Mkalama. Nakumbuka baadhi
 ya walimu walikuwa wanatumia usafiri wa baiskeli, wakifika msitu wa 
Gumanga, walikuwa wakiporwa mishahara yao na majambazi,”
Mwenyekiti huyo ambaye ni diwani (CCM) kata ya Gumanga, alisema kuwa kwa sasa hayo yote
yatabaki kuwa histori, baada ya NMB kufungua tawi hilo.
0 comments:
Post a Comment