Mkuu
wa Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida Edward Ole Lenga akizungumza na
wananchi wa kijiji cha Kinampundu mara baada ya kukabidhiwa Zahanati na
nyumba mbili za mganga na shirika moja lisilo la kiserikali la
HAPA,hafla hiyo ilifanyikajuzi kijijini hapo.
Ni
Mwakilishi wa shirika la SIMAVI kutoka nchini Uholanzi Lieke Ongering
akizungumza katika hafla ya kukabidhi mradi wake kwa ushirikiano na
shirika la HAPA Singida kukamilisha mradi wa ujenzi wa Zahanati na
nyumba mbili za mganga kijiji cha Kinampundu takribani umbali wa
kilomita 70 kutoka mjini Singida.
Ni
mmoja wa kinamama wajawazito akipimwa uzito na mkuu wa Wilaya ya
Mkalama Ole Lenga mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya zahanati hiyo,
anayeshuhudia kipimo hicho ni mhasibu mkuu wa shirika hilo Noel Makyao.
Mkurugenzi
wa HAPA Davd Mkanje (Kulia) kimkabidhi DC wa Mkalama Ole Lenga baadhi
ya vifaa vya kutolea huduma kwenye Zahanati hiyo wakati wa hafla fupi ya
makabidhiano ya mradi huo.
Ni
baadhi ya wageni kutoka Mataifa mbalimbali nje ya nchi wakicheza muziki
na wananchi wa kijiji cha Kinampundu mara baada ya kukabidhiwa mradi
huo wa afya ya uzazi wa mama na mtoto.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkalama Ole Lenga, kushoto mwenye suti, mwakilishi wa
SIMAVI, Lieke, MMkurugenzi wa shirika la HAPA, Davd Mkanje na mhasibu
mkuu wa shirika hilo Noel Makyao wakifurahia pamoja na wananchi mara
baada ya kukabidhi mradi huo.
Na Hillary Shoo, MKALAMA.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida ameonya tabia ya baadhi wananchi
kuezekea kwenye vyoo vyandarua vya kujikinga na mbu wa malaria.
Onyo
hilo limetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkuu huyo wa Wilaya,
Edward ole Lenga wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kinampundu
muda mfupi baada ya kukabidhiwa Zahanti ya kijiji na shirika la HAPA.
Alisema
imezuka tabia ya wananchi kutumia vyandarua hivyo kwa matumizi yasiyo
rasmi ikiwa na pamoja na wengine kuvifanya kama mabanda ya kuhifadhi
vifaranga vya kuku.
“Hii
ni aibu, wenzetu wanatupatia vyandarua ili tusipate malaria, nyie
mnatumia kuezeka vyoo kwa kweli hii ni aibu kubwa sana na mimi
nimetembea vijijini na kujionea hili, na kwa kweli atakayekamatwa
atakiona cha moto.” Alisema Dc Lenga kwa masikitiko.
Aidha
alisema serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kuagizi vyandarua
hivyo kwa ajili kujikinga na mbu wa malaria huku wananchi wakiziona kana
kwamba hazina msaada na kuzitumia kama kinga kwenye vyoo.
“Hivi
chandarua kukiezekwa kwenye choo si mtu unaonekana tu , acheni hii
tabia chafu, nimeunda kikosi kila kijiji atakayebainika kufanya hivyo
akamatwe na kuletwa kwangu mimi nitamshughulikia ipasavyo.” Alisisitza
Ole Lenga.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wananchi wa Wilaya hiyo
wanaoishi maeneo ya mijini kuja nyumbani na kujenga nyumba na vyoo bora.
Kwa hisani ya Mo Blog
0 comments:
Post a Comment