ZAIDI ya
shilingi bilioni 6.4 zimetumika kwa ajili ya shughuli za
matengenezo ya barabara kuu, mkoa na madaraja katika mkoa wa
Singida katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni mwaka
huu..
Kaimu
meneja wa wakala wa baraara TANROADS mkoa wa Singida Mhandisi Yohannes Mbegalo,
amebainisha hayo jana wakati akizungumza kwenye kikao cha 35 cha bodi ya
barabara.
Mhanadisi
Mbegalo amesema kuwa fedha hizo zimetumika kwa ajili ya
kugharamia shughuli za matengenezo ya kawaida kwa upande wa
barabara za lami na changarawe zilizopo mkoani Singida.
Amebainisha baadhi ya
shughuli zilizofanyika kuwa ni pamoja na matengenezo ya sehemu korofi,
matengenezo ya vipindi maalum pamoja na matengenezo ya kawaida na
kujenga makalvati.
Wakala wa barabara
mkoa wa Singida,unahudumia jumla ya kilomita 1,689.5 za barabara kuu na zile za
mkoa.
Kati ya hizo,kilomita
367.9 ni za lami sawa na aslimia 21.8 na sehemu iliyobaki yenye urefu wa
kilomita 1,321.6 sawa na asilimia 78.3 ni za barabara za changarawe na
udongo.
0 comments:
Post a Comment