
Katibu Tawala wilaya ya Mkalama Ndugu Peter Masindi amewataka watumishi wilayani Mkalama kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidi katika kuwaenzi mashujaa wa nchi waliopigana kwa ajili ya taifa la Tanzania.Kauli hiyo ametoa Julai 25, 2024 kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Mkalama wakati wa zoezi la usafi liliofanyika katika hosipitali ya wilaya ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Mashujaa nchini.Serikali inaleta fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi, tuwajibike pamoja katika kuhakikisha fedha hizi zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Kila mmoja katika nafasi yake atimize wajibu wake, huwezi kuwa shujaa kama ukishindwa kutimiza wajibu wako,...