Kijana wa kiume mkoani Singida aingiliwa kinyume na maumbile baada ya kulewa pombe na kupoteza fahamu.

KAMWELA
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kijana mmoja mkazi wa Kibaoini Singida mjini, kulawitiwa na rafiki yake baada ya kulewa pombe ya viroba aina ya jogoo.(Picha na Nathaniel Limu).
‘Ulevi noma’ hiyo imedhihirika baada vijana wawili wa kiume marafiki kunywa pombe nyingi na kuepelekea mmoja amwingilie kimwili kinyume na maumbile rafiki yake kipenzi.
Inadaiwa Athumani Juma mkazi wa Kibaoni alimwingilia kimwili kinyume na maumbile rafiki yake wa kiume mwenye umri wa miaka 26 (jina tunalo).
Kamanda wa polisi wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema tukio hilo la aina yake, limetokea Agosti 27 mwaka huu saa tatu usiku eneo la soko la Kibaoni kata ya Kindai mjini Singida.
Amesema siku ya tukio, marafiki hao walikutana dukani ambapo mtuhumiwa Athumani alinunua viroba vinne aina ya jogoo, huku muathirika akinunua viroba tisa.
Kamanda Kamwela amesema baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake, muathirika alitangaza kuwa amelewa na hivyo kila mmoja arejee  nyumbani kwao.
Kamanda kamwela amesema “Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika alimwambia rafiki yake Athumani kuwa amwache hapo ili aweze kupumzika kwa vile pombe ilikuwa imemzidi sana, lakini ghafla alianguka chini na kisha kuzirai na kupoteza fahamu”.
Amesema kuwa baada muathirika kupoteza fahamu, mtuhumiwa Athumani alitumia fursa hiyo na kuanza kumwingilia kimwili rafiki yake kinyume na maumbile.
Amesema wapita njia waliweza kushuhudia  Athumani akiendelea na unyama wake huo dhidi ya rafiki yake, lakini walipojaribu kumkamata, aliweza kuwaponyoka na kukimbilia kusikojulikana.
Kamnda huyo ameongeza kuwa “Raia wema walimbeba muathirika na kumpeleka hadi nyumbani kwao na baadae aliweza kupata  fahamu na ndipo aliposikia maumivu makali kwenye sehemu yake ya haja kubwa”.
“Baada ya muathirika kusikia maumivu makali, alikimbizwa hospitali ya mkoa na baada ya uchunguzi, alibainika ameharibiwa  vibaya sehemu yake ya siri ya kutolea haja kubwa”.
Kamwela amesema kwa sasa wameanzisha msako mkali wa kumsaka Athumani, ili waweze kumkamata na kumfikisha mbele ya mahakama kujibu tuhuma inayomkabili.

Kwa hisani ya Mo Blog
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa