Kamanda
 wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela akitoa taarifa 
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kijana mmoja mkazi wa 
Kibaoini Singida mjini, kulawitiwa na rafiki yake baada ya kulewa pombe 
ya viroba aina ya jogoo.(Picha na Nathaniel Limu).
‘Ulevi
 noma’ hiyo imedhihirika baada vijana wawili wa kiume marafiki kunywa 
pombe nyingi na kuepelekea mmoja amwingilie kimwili kinyume na maumbile 
rafiki yake kipenzi.
Inadaiwa
 Athumani Juma mkazi wa Kibaoni alimwingilia kimwili kinyume na maumbile
 rafiki yake wa kiume mwenye umri wa miaka 26 (jina tunalo).
Kamanda
 wa polisi wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema tukio hilo la aina 
yake, limetokea Agosti 27 mwaka huu saa tatu usiku eneo la soko la 
Kibaoni kata ya Kindai mjini Singida.
Amesema
 siku ya tukio, marafiki hao walikutana dukani ambapo mtuhumiwa Athumani
 alinunua viroba vinne aina ya jogoo, huku muathirika akinunua viroba 
tisa.
Kamanda
 Kamwela amesema baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake, 
muathirika alitangaza kuwa amelewa na hivyo kila mmoja arejee  nyumbani 
kwao.
Kamanda
 kamwela amesema “Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika 
alimwambia rafiki yake Athumani kuwa amwache hapo ili aweze kupumzika 
kwa vile pombe ilikuwa imemzidi sana, lakini ghafla alianguka chini na 
kisha kuzirai na kupoteza fahamu”.
Amesema
 kuwa baada muathirika kupoteza fahamu, mtuhumiwa Athumani alitumia 
fursa hiyo na kuanza kumwingilia kimwili rafiki yake kinyume na 
maumbile.
Amesema
 wapita njia waliweza kushuhudia  Athumani akiendelea na unyama wake huo
 dhidi ya rafiki yake, lakini walipojaribu kumkamata, aliweza 
kuwaponyoka na kukimbilia kusikojulikana.
Kamnda
 huyo ameongeza kuwa “Raia wema walimbeba muathirika na kumpeleka hadi 
nyumbani kwao na baadae aliweza kupata  fahamu na ndipo aliposikia 
maumivu makali kwenye sehemu yake ya haja kubwa”.
“Baada
 ya muathirika kusikia maumivu makali, alikimbizwa hospitali ya mkoa na 
baada ya uchunguzi, alibainika ameharibiwa  vibaya sehemu yake ya siri 
ya kutolea haja kubwa”.
Kamwela
 amesema kwa sasa wameanzisha msako mkali wa kumsaka Athumani, ili 
waweze kumkamata na kumfikisha mbele ya mahakama kujibu tuhuma 
inayomkabili.
Kwa hisani ya Mo Blog 
0 comments:
Post a Comment