WAJUMBE wa baraza la maoni ya Katiba mpya katika
Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, wamependekeza kuondolewa kwa kipengele cha
mgombea huru katika nafasi za udiwani, ubunge na Raisi.
Wajumbe hao
wamesema kuwa ni vyema wagombea wote wa nafasi hizo wakatokana na vyama vya
siasa, ili kupunguza uwezekano wa kumuingiza madarakani kiongozi ayesiyekuwa na
maadili mazuri.
Wakizungumza kwenye
kikao cha baraza la maoni ya katiba mpya wilaya ya Ikungi mkoani
Singida leo, baadhi ya wajumbe wamesema wagombea wanaotokana na
vyama vya siasa hupigiwa kura za maoni na kuchunjwa kwenye vikao kabla
ya kuwepewa tiketi ya kuwania nafasi husika.
Wamesema kitendo cha
kuruhusu mgombea huru, kinaweza kusababisha watu wenye ushawishi mkubwa
wa kifedha kutumia vibaya fursa hiyo kununua uongozi na kuingiza nchi
kwenye utawala wa kiditeta.
Hata hivyo Mwenyekiti wa
kikao hicho Ali Salehe amesema kuwa kuondolewa kwa kipengele hicho,
pia kunaweza kuwanyima fursa baadhi ya wagombea wazuri wanaoshindwa
kupambana na wenye fedha katika ngazi za vyama.
Baraza la maoni ya
katiba mpya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida lenye wajumbe zaidi ya 100
limemaliza vikao vyake vya siku mbili kwa kutoa mapendekezo mbalimbali
katika rasimu hiyo ya Katiba.
0 comments:
Post a Comment